Na; mwandishi wetu
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Ijumaa Machi 06.2026 imesikiliza maombi yanayotokana na shauri la madai Na.8323/2025, maombi yaliyoletwa Mahakamani hapo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu
Wajibu maobi hapo ni wadaawa wote walioko kwenye shauri la madai Na. 8323/2025 linalohusu usawa kwenye mgawanyo wa mali kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ndani ya CHADEMA ambao ni Saidi Issa Mohamed, Maulidah Anna Komu, na Ahmed Rashid Khamis ambao ni waleta maombi kwenye shauri la msingi
Sambamba na hao pia wapo Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA ambao kimsingi ni wajibu maombi kwenye shauri la msingi, linalosikilizwa mbele ya Jaji Hamidu Mwanga, ikumbukwe kuwa Lissu ambaye kwa sasa yuko gerezani kutokana na mashtaka ya uhaini yanayomkabili amefungua maombi hayo Novemba 14.2025 akiomba kujumuishwa kwenye shauri hilo kama sehemu ya wajibu maombi
Akizungumza Mahakamani hapo leo, Lissu ambaye kitaaluma ni Mwanasheria na Wakili mbobevu amesema maombi hayo yameletwa kwa njia ya chamber summons ikiungwa mkono na hati ya kiapo chake ya Desemba 12.2025, ambapo amesema hoja zinazounga mkono maombi hayo zitapanua ushahidi uliopo kwenye hati ya kiapo chake,
Lissu ameanza kwa kuzungumzia msingi wa kisheria wa maombi hayo ambapo amesema, hati ya maombi inaonesha wazi kuwa maombi hayo yameletwa chini ya masharti ya amri ya kwanza ya kanuni ya kumi (2) ya sheria ya mwenendo wa madai sura ya 33 ya sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo pamoja na vifungu vingine vya sheria husika inahusisha ‘reference to order 43 rule 2 of CPC’ inayoelekeza kwamba maombi yote kwa mujibu wa sheria hiyo lazima yawasilishwe Mahakamani kwa njia ya hati ya maombi yakiungwa mkono na hati ya kiapo cha muhusika
Amesema hoja ya msingi ipo katika amri ya kwanza ya kanuni ya pili ya sheria ambapo kupitia amri hiyo, Mahakama inaweza katika hatua yoyote ya mashauri, aidha kwa maombi ama bila maombi ya upande wowote na kwa masharti ambayo Mahakama itaona ni ya haki kuamuru kwamba jina la mdai yoyote limeongezwa kimakosa liondolewe, na kwamba jina la mtu yeyote ambaye amateakiwa kuunganishwa aidha kama mdai ama mdaiwa ama uwepo wake mbele ya Mahakama atatakiwa kuwa wa lazima ili kuiwezesha Mahakama kufanya uamuzi kwa ukamilifu/ ufanisi
Lissu ameieleza Mahakama kuwa kifungu hicho ndio msingi kama aliyosema Mahakamani hapo awali kuwa maombi hayo na kifungu hicho yanaipa Mahakama mamlaka yake ya kuamuru asiyepaswa kuwemo kwenye shauri husika aondolewe na aliyepaswa kuwepo lakini hayupo aingizwe kwa masharti ambayo Mahakama inaona ni haki ili kuiwezesha Mahakama kufanya kazi kwa usanifu
Pia kifungu hicho kinaipa mamlaka Mahakama kusikiliza na kuamua mashauri yote, sambamba na hilo ikumbukwe kuwa kifungu hicho cha mwenendo wa madai kimefanyiwa maamuzi mengi sana na Mahakama za juu, na kwamba kuna mnyonyoro mkubwa wa maamuzi juu ya kifungu hicho
Amesema mahitaji ya jambo hilo ni kuiomba Mahakama kuangalia inapokutana na maombi kama hayo, juu ya mtu anayetakiwa kuondelewa ama kuongezwa kama mdahawa
Katika kujenga hoja zake, Lissu ameialika Mahakama katika kesi ya Mussa Chande, Moza Mohammed Salim ambayo ni Civil Appeal 14, number 1, katika Mahakama ya rufani Zanzibar, kesi ya pili ni ya Stanbick Bank, Iddi Khalfan Na. 139/2021 ya Mahakama ya rufani Tanzania, Dar es Salaam
Amedai kuwa kupitia marejeo hayo imebainishwa kuwa mtu anayetakiwa aunganishwe uwepo wake ni wa lazima na bila yeye kuwepo amri ya mwisho ya Mahakama haiwezi kutolewa kwa ufanisi
Amesema Mahakama ya Rufani ilijiuliza inakuaje pale ambapo mtu huyo hajaunganishwa, ambapo kwenye hilo Mahakama ya Rufani ikasema ikarudi kwenye kesi ya TAN GAS kisha ikasema ‘its now and acceptable of the law for the court (falier is veto)’
Amedai kuwa ni kosa la msingi kutomuunganisha mdahawa katika kesi ya msingi, pia kutomuunganisha mdahawa kunaua kesi ya msingi (Veto), na katika hilo amerejea kesi ya Stanslaus Kanokola iliyoamuliwa na Mahakama ya Rufani ya Tanzania
Amesema kama ilivyo katika maombi yake, wajibu maombi wa kwanza, pili na watatu wameshikilia uzi kwamba mleta maombi asiingiie, hivyo kuhoji inakuaje kwamba wadahawa wanasema huyo asiingie wakati ni muhusika?, katika majibu yame amesema sheria haina ubishi tena pale Mahakama inapogundua kwamba mdahawa hajaunganishwa katika kesi na pande husika hazijaomba aunganishwe, Mahakama ina wajibu tofauti na huo wa kutowakubalia na kuamuru aunganishwe
Tundu Lissu amesema yeye ni mtu muhimu kuwepo katika kesi hiyo, kwani kwenye Aya ya kwanza ya hati ya kiapo ameiambia Mahakama kwamba yeye ni Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, kufuatia uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika Januari 21.2025, na kupitia uchaguzi huo hivyo yeye ndio kiongozi Mkuu wa chama
Kwenye Aya ya 2 ya ushahidi wake wa kiapo mleta maombi ameiambia Mahakama kwamba sio tu Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA bali amekuwa mwanachama wa chama hicho tangu Julai 2004, na katika kipindi chote hicho mleta maombi ameshikiria nyadhifa mbalimbali za juu katika chama chake, kama vile Mkurugenzi wa Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Chama, Makamu Mwenyekiti wa chama Tanzania Bara, ambapo katika kipindi cha takribani miaka 21 ameshikiria nyadhifa mbalimbali za chama
Katika Aya ya 3, mleta maombi amesema kwamba nje ya nyadhifa hizo amekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kwa amfululizo tangu mwaka 2004 alipojiunga na chama, na kwenye Aya ya 5 ya hati ya kiapo, mleta maombi amesema kwamba katika kipindi chote hicho kwa sababu ya kushikiliaa nyadhifa zote hizo ameshiriki na anafahamu masuala yote makubwa/ muhimu ambayo yameamuliwa na chama hicho katika kipindi cha miaka 21 ambayo amekuwa ndani ya chama
Mleta maombi anasema ameshiriki na anafahamu, kila jambo ndani ya chama hicho iwe masuala ya muungano, iwe masuala ya Zanzibar yote nk, wakati huohuo kwenye Aya ya 7, ya ushahidi wake mleta maombi anasema hao wajibu maombi wa 1, 2 na 3 anawafahamu na amefanyanao kazi kwa kipindi chote hicho isipokuwa wa 2 ni mgeni mgeni ila wengine anawafahamu fika tena kwa kipindi kirefu
Katika Aya ya 12 ya ushahidi wake, mleta maombi anasema kwa kiapo kwamba kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa chama Taifa, yeye ndiye Mwenyekiti wa vikao vyote vya maamuzi ya chama viwe vya maamuzi ya kisera ama utekelezaji wa maamuzi ya kisera, Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Taifa, vyote hivyo yeye ndio Mwenyekiti wa vikao vinavyofanya maamuzi ya chama
Tundu Lissu amesema amelazimika kuieleza Mahakama hayo yote kwakuwa ni muhimu kwa sababu shauri la msingi linazungumzia hayo, kuna sera za matendo ya kibaguzi, ukiukwaji wa sheria, maamuzi ya vikao vya chama ambavyo yeye mleta maombi ndio Mwenyekiti wake
Aidha, kwenye Aya ya 15, mleta maombi anasema shauri la msingi lililopo Mahakamani hapo linahusu uongozi wake wa chama moja kwa moja, kwa sababu shauri hilo limefunguliwa akiwa yeye ni Mwenyekiti, limefunguliwa mara tu baada ya kuwa Mwenyekiti na siku 4 tu baada ya kukamatwa na kufunguliwa kesi ya uhaini
Kwenye Aya ya 16, mleta maombi anasema kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa chama ndiye anategemewa kutekeleza uamuzi wowote utakaotolewa na Mahakama hiyo
Pia, amesema yeye kama Mwenyekiti ndio atasimamia maamuzi ya chama, hata kama suala la mgawanyo wa mali, kwahiyo utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama hiyo unamtegemea yeye kwa nafasi yake
Aya ya 17, mleta maombi anasema maamuzi yoyote (advace) hukumu, uamuzi ama amri yoyote ya Mahakama dhidi ya mlalamikiwa na mjibu maombi wa 4 na 5 ambao ndio wadahawa katika shauri la msingi utamuathiri yeye moja kwa moja
“Mheshimiwa Jaji amri yoyote ambayo utaipitisha ambazo zimeombwa ukikubali maombi kwamba shughuli za chama zisimame maana yake ni kwamba Mwenyektii hatoweza kuongoza vikao ikiwemo Mkutano Mkuu, hivyo ni moja kwa moja ataathirika na uamuzi wowote iwe hukumu, uamuzi ama amri itakayotolewa, Mheshimiwa Jaji huo ndio ushahidi uliopo mbele yako uliotolewa kwa kiapo” -Lissu
Aidha, Lissu amedai kuwa katika ushahidi huo ni wazi kuwa yeye kama mleta maombi ni mdahawa wa lazima, na amesema hayo kwa kutumia maneno ya Mahakama ya Rufani katika maamuzi aliyoyasema kwamba yeye ni mdahawa wa lazima, na kwamba haepukiki kuwepo kwenye kesi hiyo kwakuwa ni mtu muhimu sana, na Mahakama ya rufani imesema kwamba mdahawa wa aina kama yake ni muhimu
“Kwa ushahidi huu, order 1 rule 2 inasema Mahakama imuingize kwa masharti ambayo Mahakama itaona ni ya haki, rai yangu kama mleta maombi ni kwamba Mahakama hii iamuru kwamba mleta maombi aingizwe, hili suala lina maslahi makubwa sana katika umma wa nchi hii sio suala la kupatiwa pesa, uamuru mleta maombi aingie kama mdahawa na kila upande ubebe gharama zake, rai yangu ukubali maombi na kila upande ubebe gharama zake” -Lissu.