Latest Posts

TUPENI KURA ILI TUINUE HESHIMA NA UTU WA MTANZANIA- DKT. SAMIA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaomba wananchi wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni leo Alhamisi Septemba 11, 2025, Dkt. Samia amesema kura za wananchi ndizo zitakazowezesha utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na chama hicho kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

“Ili tuweze kuyafanyia kazi tuliyoyaahidi ninawaomba sana Wanakaliua, kila aliyejiandikisha kupiga kura, mtoke kwa wingi namna hii kama mlivyotokea hapa. Mwende mkakipigie kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili tuweze kutekeleza haya tunayoyaahidi,” amesema.

Ameongeza kuwa CCM imejidhihirisha kwa vitendo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo, na kwamba wananchi wanapaswa kuendelea kukiamini chama hicho kwa kura zao.

“Kwa upande wetu hatuna wasiwasi wa kuyatekeleza, kwa sababu tulishatoa mfano miaka mitano iliyopita, tumetekeleza na mmeona, na mbele hapo tutakwenda kutekeleza ili kuinua utu na heshima ya Mtanzania,” amesisitiza Dkt. Samia.

Aidha, amewaomba wananchi wa Kaliua kuhakikisha wanawapigia kura wagombea wote wa CCM kuanzia ngazi ya urais, ubunge hadi udiwani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!