Latest Posts

TUWAKATAE WANAONUFAIKA NA VURUGU- KAZAZI

Vijana na Watanzania kwa ujumla wametakiwa kujiepusha na kutumika na watu wachache wenye kutanguliza maslahi yao binafsi ambao wamekuwa wakipata kipato kutokana na uharibifu, vurugu na ghasia wanazozihamasisha kufanywa ndani ya Jamii ya Watanzania.

Wito huo umetolewa na Bw. Juma Rashid Kazazi, Mkazi wa Dar Es Salaam wakati akizungumza kuhusu kadhia ya vurugu, wizi na uharibifu uliotokea Oktoba 29, 2025 na baada ya siku ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akisema wapo wanaonufaika na ghasia hizo huku washiriki wa ghasia hizo wakiathirika.

“Ndugu zangu Watanzania sasa tusifikie Vijana tukawa ni sehemu ya kipato cha watu, mtu anakuja kwa maslahi yake. Hilo jambo nawasisitiza Vijana wa Kitanzania mjaribu kukaa, mfikirie na si kila jambo ni la kupokea maana katika matukio haya wanatengenezea watu kipato na sisi tunabaki kuumia, kushinda njaa, kupigwa na hata kufa.”

“Wao wanafaidika sisi tunaendelea kuumia na ni muhimu tujifunze kwa tukio lile na kama wana nia njema waje na wao tushirikiane kwenye kuandamana badala ya kututanguliza sisi wakati wao wapo nje ya nchi. Niwaombe Vijana hili jambo tuliangalie kwa ukubwa na tuwakatae watu hawa na kile wanachotuambia.” Amesema Bw. Kazazi.

Akieleza kuwa ni mara ya kwanza kushuhudia uharibifu na vurugu zile, amewaomba watanzania pia kukemea jambo hilo jipya nchini, akisema ikiwa Watanzania wote watasimama pamoja watafanikisha kuidumisha amani ya Tanzania na kuruhusu kila mmoja kuendelea na shughuli zake za kiuchumi na kijamii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!