Latest Posts

UMOJA WA ULAYA KUTAFUTA SULUHU NA CHINA ALHAMISI

Na Vanessa Sindato

Viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen na Antonio Costa, wamewasili jijini Beijing wakilenga kuendesha mazungumzo ya kisiasa na ya kibiashara na wakuu wa serikali ya China. Mkutano huo unatarajiwa kuangazia mvutano wa kibiashara na mzozo wa Ukraine, ingawa matarajio ya kupatikana kwa mwafaka yameonekana kuwa ya kiwango cha chini.

Kutokana na taarifa iliyoripotiwa na DW, viongozi hao wamewasili wakisindikizwa na Kaja Kallas, mwanadiplomasia mashuhuri wa Umoja wa Ulaya. Video kutoka vyombo vya habari vya China zimewaonesha Von der Leyen, Costa, na Kallas wakifika katika mji mkuu wa China kwa mazungumzo ambayo yamepangwa kufanyika na Rais Xi Jinping pamoja na Waziri Mkuu Li Qiang.

Costa

Maafisa kutoka Brussels wamesema kuwa mazungumzo hayo ni fursa adhimu ya kuimarisha uhusiano na China kwa kuchukua hatua za msingi na za kina katika maeneo yenye mvutano.

Umoja wa Ulaya unatarajia kuweka wazi msimamo wake kuhusu masuala kadhaa muhimu yanayohusiana na biashara, teknolojia, na usalama wa kimataifa.

China kwa upande wake imekuwa ikionesha nia ya kukuza ushirikiano na Umoja wa Ulaya, ikijiweka kama mshirika wa kuaminika na thabiti katika mazingira ya kimataifa yenye changamoto.

Beijing inajaribu kuonesha kwamba inaweza kuwa mbadala imara kwa mataifa ya Magharibi, hususan Marekani, katika masuala ya kibiashara na kisiasa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!