NA Theophilida Felician.
Shirika la umoja wa kikiristo hapa nchini la UNITY CHRISTIAN INTERNATIONAL limedhamiria kuunga mkono serikali kwa kusaidia ujenzi wa huduma za kijamii hususani shule na hospitali.
Ametoa kauli hiyo rais wa shirika hilo prof Wilson George Munguza wakati akizungumza na chombo hiki akiwa makao mkuu ya shirika mkoani Dar es salaamu.
Amesema kuwa shirika hilo limeanzishwa hapa nchini kwa lengo kuu mahususi lakuimarisha umoja wa makanisa yote ya kikristo kwakuongeza mshikamano na upendo kwa waumini wa kikiristo.
Prof Munguza amesema kuwa shirika linajikita zaidi kuunga mkono juhudi za serikali katika kupaza sauti nakuuleta umoja kwa jamii nakuongeza ujenzi wa miundo mbinu ya shule na hospitali kwani ni hitajio lililo muhimu zaidi kwa wananchi.
Hata hivyo ameongeza kwamba shirika hilo ambalo linafanya kazi zake hapa nchini na Afrika mashariki na kwingineko litaendelea kuzitumia njia mbalimbali ili kuwafikia wananchi ikiwemo ya makongamano, mikutano, vyombo vya habari na nyinginezo nyingi huku akihimiza jamii kwa ujumla kudumisha amani, upendo na mshikamano nyakati zote.
