Latest Posts

SHAHIDI BODABODA ‘MWANACHADEMA’ ADAI KUSHAWISHIWA NA LISSU KUZUIA UCHAGUZI

Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu tayari imeanza katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam ambapo upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Renatus Mkude umeieleza mahakama kuwa kutakuwa na mashahidi wanaolindwa(mashahidi wa kificho) na mashahidi ambao hawalindwi(askari kutoka majeshi tofauti tofauti).

Shahidi wa kwanza ni wa kificho aliyejitambulisha kama Dereva Bodaboda ambae ni Mkristo, mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Songea Ruvuma ameanza kutoa ushahidi akiongozwa na Wakili wa Serikali Cathbeth Mbilinyi.

Ameieleza mahakama kuwa mwezi oktoba 2024 alianza kushiriki siasa za chama cha CHADEMA kwa kushiriki mikutano ya hadhara na kwa kufuatilia baadhi ya viongozi ili aweze kuwafahamu

Kwa kipindi hiko alifanikiwa kuwafahamu baadhi ya viongozi akiwemo Mhe. Lissu na baadhi ya viongozi walikuwepo songea alimfahamu Katibu wa vijana wa Songea ambapo kwa wakati huo alikuwa kwa jina la Chiza maarufu kama Mwamba wa Kigoma

Mwezi Januari 2025 baada ya kushiriki na kuanza kuhudhuria mikutano ya CHADEMA ilipofika mwaka huo akavutiwa na kutaka kuwa mwanachama wa chama hicho. Ndipo akaanza jitihada za kutafuta viongozi ambao wapo sehemu alipo kuonesha nia yake ya kutaka kuwa mwanachama wa CHADEMA ndipo akamfata kiongozi wa Wilaya ambae ni Chiza maarufu kama Mwamba wa Kigoma na kumueleza nia yake ya kutaka kuwa mwanachama

Alisifiwa kwa uamuzi mzuri na akaambiwa ili kuwa mwanachama lazima awe na kadi ya chama, akaambiwa atafanyiwa utaratibu wa kupata kadi na kuanzia wakati ule atakuwa anamshirikisha kwenye shughuli mbali xa chama ili waweze kuwa pamoja

Akaambiwa kwa wakati huo utaratibu wa kuapta kadi unasumbua kwa sababu mashine ya kupata kadi ilikuwa mbovu aendelee kusubiri ikiwa tayari atapata kadi.

 

Tarehe 4/4/2025

Anasema tarehe hiyo akiwa sehemu yake ya kazi na akiwa na  simu yake ya mkononi aina ya Infinix Smart 8 akiwa anaangalia mtandao wa YouTube ambao amedai ni mtandao wa kijamii unaomuwezesha mtu kutuma video, audio na maudhui mengine anaeleza aliweza kuingiza kwenye mtandao huo. Na simu yake ilikuwa na bando la internet pia aliingia kwenye app ya google ambayo inamuwezesha kuingia moja kwa moja YouTube

Alifanikiwa kuingia kwenye akaunti au chaneli ya Jambo TV  kusikiliza hotuba ambayo alikuwa anatoa Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA ambapo alikuwa akihutubia ambapo alimuona na kumsikia akihutubia watu kwamba “bila mabadiliko hakuna uchaguzi hivyo tunaenda kukinukisha tunakwenda kuvuruga uchaguzi pia nilisikia na kuona akisema tunakwenda kukinukisha yeyote ambae atakua pamoja nasi tutaenda nae ambae hatotaka tutamua kama kuna mtu yeyote ambae anatarajia kugombea udiwani asahau, yeyote ambae anatarajia kugombea ubunge pia asahau, hata mimi Mwenyekiti kuhusu kugombea Urais hiyo sahau, bila mabadiliko hakuna uchaguzi, pia akasema wanasema tunafanya uasi anasema ni kweli utakuwa uasi bila mabadiliko hakuna uchaguzi”

Anasema mazingira aliyoyaona yalikuwa ya ukumbini sehemu aliyosimama(Lissu) nyuma ya ukuta kilionekana kitambaa ambacho kilikuwa na rangi ya bendera yenye rangi za Tanzania na bendera yenye rangi za CHADEMA kwa pembeni.

Lissu alikuwa amevaa kombat ya kaki, anamfahamu Lissu kama mwanasiasa mkongwe na maarufu. Baada ya kusikiliza video ya Lissu kwa makuni maneno yake yalimwingia moyoni na yalimshawishi  na kutamani kuwa miongoni mwa watu ambao watashiriki au wataunga mkono ajenda ya kuzuia uchaguzi pasipo mabadiliko kuzua uchaguzi kwa maana ya kukinukisha

“Ajenda ya kukinukisha ni kwamba mimi kufanya vurugu au kuharibu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 unaohusisha uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais” shahidi

Anaeleza baada ya kushawishika aliamua kumfata Mwenyekiti wa Vijana ambae alikuwepo Songea wakati huo alikuwa ndugu Chiza maarufu kama Mwamba wa Kigoma

Akamueleza kuwa alishawishika na Mwenyekiti na kutamani kuwa miongoni mwa ambao watakinukisha ili kutaka mabadiliko kabla ya uchaguzi baada ya kumwambia Chiza alimsifia kwa uamuzi mzuri

Baada ya hapo akaahidiwa kuwa chochote ambazo kitaendelea kuhusiana na harakati hizo za kukinukisha atamshirikisha akamuahidi atamuanganixha na ma group mbalimbali ambayo yanajadili mipango hiyo hiyo

Anasema anakumhuka group ambalo alifanikiwa kuwepo ni group la ‘SIASA YETU UPDATE

 

TAREHE 06/04/2025

Anahadithia shahidi kuwa siku hii alipata taarifa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA (Lissu) atakuwa na ziara mkoani Ruvuma akipata taarifa kutoka kwa Chiza

Aprili 6,2025 shahidi alidai alipata taarifa kuwa Lissu atakuwa na ziara katika Mkoa wa Ruvuma na taarifa hiyo aliipata kutoka kwa Chiza alidai taarifa iliwataka kufanya maandalizi kwa ajili ya kumpokea Mwenyekiti wao Lissu.

Alidai walianda maandalizi na wakapanga Aprili 10,2025 Lissu atakuwepo Songea katika uwanja wa shule ya Msingi Matarawe Songea Mjini.

Shahidi alidai Aprili 9,2025 alipata taariga kuwa mwenyekiti amekamatwa huko Wilaya ya Mbinga akiwa kwenye ziara na baada ya kupata taarifa hiyo alienda kumuuliza Chiza kuwa anasikiaLissu amepakamatwa huko Mbinga.

Shahidi alidai baada ya kumuuliza Chiza alimwambia ni kweli kuwa Lissu amekamatwa lakini ratiba ya mkutano wa Aprili 10,2025 itakuwepo palepale alimtaka ajiandae ili siku hiyo wawepo kwenye mkutano.

Shahidi alidai ilipofika tarehe tajwa walikusanyika katika uanja wa shule ya Msingi Matarawe ili kusubiri viongozi waliokuwa katika msafara wa mwenyekiti waweze kuhutubia kwenye Mkutano.

Alidai viongozi hao alikuwepo Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche, Godbless Lema na Dk Wilbroad Slaa wakati wakisubiri ilitokea gari la polisi na kuwatawanya ikieleza kuwa hakutakuwa na mkutano siku hiyo, hivyo haruhusiwi mtu yeyote kukaa eneo hilo.

Shahidi alidai baada ya katazo la Polisi walitawanuika na kuelekea ofisi za chama zilizopo katika eneo la Mfaranyaki Songea  ili kufahamu kinachoendelea kwa siku hiyo na baada ya kufika hapo waliona waandishi wa habari wakijianda kufanya mahojiano na viongozi katika ofisi hizo.

Alidai kuongozi anayekumbuka alikuwepo katika eneo hilo ni Ade Mayalla ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini

Alisikia polsii wanasema hatakiwi mtu yeyote kuonekana kwenye ofisi hiyo hivyo watawanyike anaeleza haada ya kutawanywa kwenye ofisi hizo akaelekea shule ya msingi ya … baada ya hapo alifika kiongozi ambae ni Makamu Mwenyekiti na kusema  amepokea barua kutoka Polisi kwamba kwa siku hiyo usifanyike mkutano wowote katika eneo hilo  akawaambia watawanyike viongozi watapanga tarehe nyingine kwa ajili ya mkutano huo

 

TAREHE 18/4/2025

Shahidi anasema akiwa kwenye shughuli zake kuwa tarehe 20/04/2025 siku ya Pasaka kutakuwa na matembezi ya hiyari ambapo kwenye matembezi hayo yataambatana na kuvaa t-shirt zilizoandikwa No Reform No Election ukafanykka utaratibu unachangia 10k na t-shirt zinasafirishwa kutoka Dar Es Salaam hadi kukufikia wakakubaliana ifikapo siku hiyo wakutane kwa ajili ya matembezi hayo ya hiyari.

T-shirt zilifika na kila mmoja alipata t-shirt yake jioni saa 10 ndio yatafanyika matembezi ya hiyari taarifa hizo wakipewa kwenye group siasa yetu.

Anasema walikubaliana wakutane Songea mjini sehemu inaitwa kwa Diss Kitimoto. baada ya kusogea eneo hilo bodaboda wakisogea waksiubiri wengine likata gari la Polisi akiwa amevaa t-shirt ya no reform no election.

Polisi wakajitambilisha na kuwaambia wanahitajika kituoni kwa ajili ya mahojiano wakawakamata na kuwaweka kwenye gari hadi kituo cha polisi Songea wakaambiwa wanashtakiwa kwa tuhuma za kupanga maandamano bila kibali. Wakaambiwa watatoka kwa lakini ifikapo tarehe 25/4/2025 wanatakiwa kuripoti ofisi ya RCO Ruvuma tukaripoti ofisi ya RCO Ruvuma akawataka kueleza ilivyokuwa mpaka kufikia hapo

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!