Latest Posts

VIFO VYA WAANDAMANAJI IRAN VYAZIDI KUSHTUA: EU YASEMA ITACHUKUA HATUA KALI DHIDI YA TEHRAN.

Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza kujiandaa kuweka vikwazo vipya na vizito dhidi ya Serikali ya Iran kufuatia kile walichokiita matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wanaandamana kuipinga serikali hiyo.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, amelaani vikali hatua za utawala wa Iran kukandamiza uhuru wa raia, akisisitiza kuwa Umoja huo unasimama bega kwa bega na wananchi wanaopigania haki zao. Kupitia taarifa yake, Von der Leyen ameeleza kushtushwa na ongezeko la vifo ambalo limefikia kiwango cha kutisha tangu maandamano hayo yaanze mwezi Desemba 2025.

Msemaji wake, Paula Pinho, amethibitisha kuwa msimamo wa EU uko wazi na mchakato wa kuangalia vikwazo zaidi unaendelea. “Tunaangalia uwezekano wa kuweka vikwazo zaidi,” alisema Pinho, akiashiria kuongezeka kwa shinikizo la kimataifa dhidi ya Tehran.

Maandamano hayo yaliyolipuka Desemba 28 kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu ya riale na ugumu wa maisha, sasa yamegeuka kuwa vuguvugu kubwa la kitaifa linalotaka mabadiliko ya mfumo wa utawala. Hatua hii ya Umoja wa Ulaya inaungana na shinikizo lingine kutoka kwa Marekani, ikionesha kutengwa zaidi kwa utawala wa Iran katika jukwaa la kimataifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!