Watanzania wawili wamejishindia bodaboda mbili katika droo ya promosheni ya kampuni ya michezo ya kubahatisha ya PigaBet iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kampeni maalum ya kuwazawadia wachezaji wake.
Akizungumza baada ya droo hiyo, Afisa Masoko wa PigaBet, Hemed Msonge, alisema kampuni hiyo imeanza rasmi mpango wa kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia zawadi za bodaboda mbili zitakazotolewa kila wiki kwa muda wa wiki sita mfululizo.

Alisema promosheni hiyo inalenga kuwapa wateja fursa ya kujiongezea kipato kupitia usafiri wa bodaboda huku ikiendelea kuwahamasisha kushiriki michezo kwa uwajibikaji.
Msonge aliwahimiza Watanzania wengi zaidi kushiriki promosheni hiyo akisema, “Cheza, shinda bodaboda na ubadilishe maisha yako,” huku akisisitiza kuwa droo zitaendelea kufanyika kila wiki hadi mwisho wa kampeni hiyo.