Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Jumatatu Julai 15.2024 amekagua na kuzindua mitambo na vifaa vipya vya kurushia matangazo vya kampuni ya Azam Media Limited
Vifaa hivyo ni pamoja na magari ya kisasa ya kurushia matangazo (OB Van), kamera za kisasa pamoja na mfumo wa kusaidia maamuzi viwanjani (VAR), ambapo vifaa hivyo vilivyogharimu shilingi bilioni tano vitatumika katika kurushia matangazo ya mpira wa miguu wa ligi Kuu Tanzania bara na Zanzibar pamoja michezo mingine
Akizungumza na wafanyakazi wa Azam media pamoja na wadau wa michezo waliojitokeza kwenye hafla hiyo Majaliwa amesema manunuzi ya vifaa hivyo ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari kwani kunaifanya Tanzania kuwa nchi ya kipekee kuwa na vifaa vya kisasa vya aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki
Majaliwa pia ameshuhudia uzinduzi wa chaneli mpya ya Azam 4 HD ambayo itatumika kurusha ligi kuu ya Ufaransa (Legue 1) na ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga)