Latest Posts

WALIPAKODI BORA 1228 KUKABIDHIWA ZAWADI NA RAIS DK. SAMIA JANUARI, 23, 2025

Jumla ya Walipakodi 1228 kutoka kona zote za Tanzania, wanatarajia kukabidhiwa zawadi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi itakayofanyika Januari 23, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini humo tarehe 22 Januari 2025 Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo amesema zawadi hizo zitatolewa kwa walipakodi waliyofanya vizuri katika kulipa kodi kwa kipindi cha Julai 2023 mpaka Juni 2024.

Kayombo ametaja vigezo walivyotumia kuwachagua wanaopewa zawadi ikiwemo mlipakodi kodi mwenye rekodi nzuri katika ulipaji wa kodi, mlipakodi kwa hiari na kwa wakati, mlipakodi anayetumia EFD mashine kikamilifu, mlipakodi aliyelipa kodi kubwa zaidi na mlipakodi anayetoa ushirikiano kwa TRA.

Kayombo amesema zawadi hizo zitachagiza walipakodi wengine kufanya vizuri zaidi ili na wao watunukiwe wakati ujao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!