Latest Posts

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WENYE MAADILI MEMA

Vijana wametakiwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa kuchagua viongozi wenye maadili mema na wanaopinga vitendo vya rushwa, ambavyo vimekuwa kikwazo katika kupata viongozi sahihi ndani ya jamii.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa kutoka Mkoa wa Geita, Reuben Sagayika, wakati akizungumza katika kongamano la vijana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Maria Goleth, mjini Geita.

Sagayika amesema ni muhimu kwa vijana kutumia nafasi yao ipasavyo kwa kuwachagua watu waadilifu, wenye hofu ya Mungu na wenye maono ya kuleta maendeleo katika maeneo yao.

“Vijana tunayo nafasi ya kubadilisha taswira ya uongozi nchini kwa kuchagua viongozi wanaojali maslahi ya wananchi na siyo wale wanaotafuta madaraka kwa ajili ya kujinufaisha kupitia vitendo vya rushwa,” amesema Sagayika.

Aidha, amewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani na mshikamano kipindi chote cha uchaguzi ili kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa utulivu na haki.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!