Latest Posts

MPINA NA MKAKATI WA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU JIMBO LA KISESA

Katika kuhakikisha mkakati wa kushuhudia wanafunzi wanafanya vizuri kwenye sekta ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Mbunge wa jimbo la Kisesa, lililopo wilayani Meatu mkoani Simiyu Luhaga Mpina (CCM) ameendelea na ziara yake ya kuhakikisha anafikia shule zote za sekondari zilizoko jimboni humo na kukabidhi mashine za kuprint na kutoa copy (computers machine) ambazo zitatumika kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia kwa walimu na wanafunzi wa shule hizo.

Akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Sakasaka ambayo ni sehemu ya shule tisa (9) za awali zilizofikiwa na mradi huo Mpina ameeleza matumaini yake kuwa anaamini sasa wanafunzi wa jimbo hilo watafanya vizuri zaidi katika mitihani ijayo

Amesema wakati anaingia kuongoza Jimbo hilo kwa mara ya kwanza kulikuwa na shule moja pekee ya sekondari ambayo ni shule ya sekondari Mwandoya iliyopo mji wa Mwandoya ambao ni makao makuu ya jimbo la Kisesa, lakini kwa sasa jimbo hilo lina shule za sekondari 17 jambo ambalo amesema ni upigaji mkubwa wa hatua za maendeleo

Amesema huko nyuma wanafunzi walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata shule jambo ambalo lilipelekea wengi wao kushindwa kumaliza shule kutokana na uwepo wa sababu mbalimbali ikiwemo hali za kiuchumi za familia, kupata ujauzito kwa baadhi ya wanafunzi wa kike kutokana na ushwishi kutoka kwa watu wasiokuwa wema nk, jambo ambalo kwa sasa hatarajii kulisikia kwa kuwa shule zipo  karibu na walimu wapo hususani walimu wa masomo ya sayansi ambao kipindi cha nyuma walikuwa adimu kupatikana

Aidha, Mpina pamoja na mambo mengine ametumia jukwaa hilo kurusha jiwe gizani kwa baadhi ya viongozi wa kuchaguliwa wakiwemo Madiwani na Wabunge wanaotumia madaraka na nafasi zao kujinufaisha wao binafsi, rafiki zao na familia zao jambo ambalo kwake ameapa kuwa hawezi kulifanya

Akitoa salamu kwenye hafla hiyo baada ya kufika eneo la Sakasaka, Diwani wa eneo hilo amemshukuru Mbunge Luhaga Mpina kwa kufikisha kilio na kero zao kwa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye mara zote amekuwa msikivu na mtatuzi WA kero zao mbalimbali hususani zile zinazotoka kwenye kamati ya ushauri ya kata (WADC) na kupelekwa ngazi za juu kwa ajili ya utekelezaji

Akiwa hapo, Diwani huyo amemuomba Mbunge Luhaga Mpina kuendelea kuwapigania ili Maabara ya shule ya sekondari ambayo haijaanza kufanya kazi mpaka sasa kutokana na kukosekana kwa vifaa mbalimbali licha ya uwepo wa jengo lake ianze kufanya kazi ili ichochee wigo kwa wanafunzi kufanya vizuri zaidi katika masomo na mitihani yao

Pia, ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani na pongezi kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya na kwamba licha ya changamoto wanazokabiliananazo zinazotokana na uchanga wa shule, lakini wahakikishe mitihani iliyoko mbeleni wanafanya vizuri zaidi

Wakizungumzia zoezi hilo baadhi ya maafisa kutoka Halmashauri ya wilaya ya Meatu akiwemo Joseph Malaika ambaye ni Afisa TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) amesema katika mashine zilizokabidhiwa kila moja ina uwezo wa kutoa copy na kuprint, sambamba na hilo amesema mashine hizo kila moja ina uwezo wa kutoa karatasi 150 ndani ya dakika moja

Wataalamu hao wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu akiwemo Afisa Elimu wametoa msisitizo kuwa mashine hizo zimetolewa mahsusi kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia pekee na kwamba zisitumike kwa matumizi mengine kinyume na yaliyokusudiwa

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wazazi na walezi walioshuhudia hafla za makabidhiano hayo akiwemo Ibrahim Mkalango Nchama Kiruma wamemshukuru Mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina kwa kukabidhi mashine hizo katika shule mbalimbali ambapo wameeleza kuwa zitasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha ufaulu kwa watoto hao

Sambamba na hilo, wazazi na  walezi hao wametoa wito kwa walimu na wanafunzi kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa huku wakitoa wito wa utunzaji ili vidumu kwa muda mrefu na kusaidia watoto wao kuongeza wigo wa kuijuwa TEHAMA

Katika hatua nyingine wazazi na walezi hao wakiwa sehemu ya wakazi wa jimbo la Kisesa wamemshukuru Mbunge huyo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali ya CCM kwa ujumla wake kwa kufanikisha maendeleo jimboni humo ikiwemo kufikishiwa kwa huduma ya umeme, Barabara zilizopo zinapitika kwa nyakati zote nk

Jina la Mbunge wa jimbo la Kisesa (CC) Luhaga Joelson Mpina limekuwa likitajwa sana hapa nchini hivi karibuni kutokana na kuibua sakata la uagizaji wa vibali vya sukari kutoka nje ambapo yeye anadai kuwa serikali ilikengeuka kwenye maeneo kadhaa hali iliyopelekea kufungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge huku yeye akifungua kesi za kupinga jambo hilo Mahakamani akiilenga serikali na Bunge kupitia Mawaziri wa Kilimo Hussein Bashe, na Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba bila kuwasahau Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Bodi ya Sukari Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na baadhi ya makampuni binafsi anayodai yamehusika kwenye mpango huo

Wakati huu akisubiri hatma ya kesi zake alizofungua Mahakamani zinazotarajiwa kuanza kurindima hivi karibuni Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kwa sasa Mbunge huyo machachari ameweka kambi jimboni kwake akifanya mikutano kadhaa na kukutana na wapiga kura wake.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!