Latest Posts

WAKULIMA WATAKIWA KUZINGATIA UBORA WA ZAO LA MBAAZI ILI WAPATE BEI NZURI

Vyama vya Msingi vinavyosimamiwa na Chama Kikuu Cha Ushirika kinachohudumia wilaya za Mtwara, Masasi na Nanyumbu (MAMCU LIMITED) mkoani Mtwara vimetakiwa kutochelewesha malipo kwa wakulima na badala yake waharakishe ili kuondokana na malalamiko yasiyokuwa ya lazima.

Hayo ameyazungumza Mwenyekiti wa Mamcu, Alhaji Azam Mfaume kwenye mnada wa pili wa zao la mbaazi ambapo wameuza tani 2,552 za mbaazi kwa bei ya juu shilingi elfu 1,900 na bei ya chini shilingi elfu 1,850.

Amesema tayari wanunuzi wameshalipa fedha za mnada wa kwanza na wao wameshapeleka kwenye vyama hivyo vya msingi (AMCOS) hivyo amewataka viongozi kuharakisha malipo hayo yanafanyika kwa wakati.

Kwa upande wake Meneja wa Mamcu, Biadia Matipa amewaomba wakulima kuzingatia ubora ili waendelee kupata bei nzuri kwenye soko hilo.

“Tumeona ni vyema kuongeza idadi ya minada ili tuweze kufanya minada mingi kabla ya kufika mwezi Septemba 2024 pamoja na kuwahi bei nzuri ambayo ipo sokoni, minada hiyo itakuwa inafanyika mara mbili kwa wiki kila jumanne na ijumaa”, amesema Matipa.

Nae Afisa Usimamizi wa Fedha wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Prince Mng’ong’o amesema kushuka kwa bei kwenye mnada huo wa pili ni kutokana na idadi ndogo ya wanunuzi iliyosababishwa na kushtukizwa kwa mnada huo.

“Naomba niwahakikishie wakulima kuwa bei hizi zitaimarika kwenye minada inayofuata kwasababu ratiba hii itaenda kuwafikia wanunuzi wote kuwa chama cha Mamcu kitakuwa kinafanya mnada kwa siku mbili”, amesema Mng’ong’o.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!