Latest Posts

TEA NA TOTALENERGIES MARKETING TANZANIA LTD ZAJADILI USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA ELIMU

Wawakilishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd leo tarehe 27 Agosti 2024 wamekutana kwa lengo la kuona namna wanavyoweza kutekeleza kwa ushirikiano miradi ya kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia hapa nchini.

Mkutano huo umefanyika Makao Makuu ya TEA, Ilazo Jijini Dodoma na kuongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, CPA Mwanahamisi Chambega ambapo amesema TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd imekuwa mdau wa TEA wa muda mrefu na kwamba TEA iko tayari kuendelea kushirikiana nao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano ya kampuni wa TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd Bi. Getrude Mpangile amesema katika mwaka huu kampuni hiyo ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd imetengeneza madawati 200 yenye thamani ya Sh. Milioni 25.9 ambayo yatanufaisha wanafunzi 600 katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Bi Mpangile ameongeza kuwa mradi mwingine unaotekelezwa na TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd katika mwaka huu ni ule wa kuwezesha wanafunzi wa kike mashuleni ukijikita katika kutoa taulo za kike.

Jumla ya Katoni 500 zenye thamani ya Sh. Milioni 35.4 zimelengwa kusambazwa kupitia mradi huo wa taulo za kike.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!