Zaidi ya mashirika binafsi 60 kati ya 499 yamefutiwa usajili mkoani Morogoro kutokana na kushindwa kuwasilisha taarifa zao binafsi na za maendeleo Serikalini
Hayo yamebainishwa na Afisa maendeleo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Delfina Pacho katika jukwaa la mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo amesema kuwa licha ya mashirika binafsi kuwa na msaada mkubwa katika jamii lakini kunabaadhi ya mashirika yamefutiwa usajili kutokana na kutokutuma maarifa katika mfumo kwa muda mrefu.

“Mashirika binafsi kwa Mkoa wa Morogoro yapo takribani 499 ili mashirika zaidi ya 60 tumeamua kufuta usajili wao na kusitisha kutokana na kutokutuma taarifa zao binafsi katika mfumo kwa muda mrefu pia hayalipi ada ya mwaka pamoja na ukosefu wa elimu”, ameeleza Pacho.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Morogoro Musa Kilakala ameyataka mashirika hayo kutoa taarifa zao kwa uwazi pamoja na kufanya kazi kwa kufata misingi ya nchi.