Naibu Waziri wa habari, mawasiliano na Teknolojia ya Habari, MaryPrisca Mahundi amesema serikali inaendelea kutafuta njia bora zaidi ya kuruhusu watoa huduma za usajili wa laini za simu kuweza kuwafikia wananchi bila kuathiri viwango vya usalama na udhibiti.
Mahundi ametoa kauli hiyo bungeni Dodoma mara baada ya Mbunge wa Makete Festo Sanga kuhoji haja ya serikali kusitisha usajili wa laini za simu kiholela mitaani na badala yake watu wajisajili kwenye maduka maalum ya mitandao ya simu kama nchi jirani wanavyofanya ili kudhibiti utapeli ambao umekuwa ukiumiza na kugharimu Watanzania.
“Lengo ni kuhakikisha usalama na uthibiti ubora wa huduma hizi. Tutaendelea kutafuta njia bora zaidi za kuwaruhusu watoa huduma kuwafikia wananchi bila kuathiri viwango vya usalama na uthibiti.” Amesema Waziri Maryprisca.