Latest Posts

MKUTANO WA OACPS DAR ES SALAAM: PM MAJALIWA AONGOZA MAJADILIANO YA USIMAMIZI WA BAHARI NA UVUVI

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa tarehe 11 Septemba 2024, amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) unaohusika na masuala ya Uvuvi, Bahari, Maziwa na Mito.

Mkutano huu unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam unalenga kuimarisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na nchi wanachama, kuboresha usimamizi wa rasilimali za bahari, na kuendeleza uchumi wa buluu.

Vilevile, mkutano huu unahimiza kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya usimamizi wa uvuvi endelevu.

Aidha, mkutano huo unatarajiwa kutoa mwongozo wa kimkakati kwenye vikao vya juu vya maamuzi vya Umoja wa Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS), ili kusaidia kuboresha na kudhibiti sekta ya uvuvi, ufugaji samaki, na usimamizi wa bahari kwa maendeleo endelevu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!