Latest Posts

KUHUDUMIA WATEJA NA UTOAJI WA TAARIFA KWA WAKATI VYAIPA TUZO TANESCO TENA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeshinda tena tuzo kutoka JamiiForums kwa utoaji wa majibu ya changamoto za wateja kwa wakati ,kuzifanyia kazi pamoja na utoaji wa taarifa mbalimbali.

Kupitia ukurasa hai (Thread ya TANESCO) inayoendeshwa kwenye jukwaa la Jamii Forums, Tanesco wamekua wakijibu na kutoa suluhisho la matatizo mbalimbali ya wateja wanapopata changamoto za upatikanaji wa umeme nchini.

Tuzo hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita zikihusisha taasisi mbalimbali za serikali pamoja na viongozi walio mstari wa mbele kwenye kutatua kero za Wananchi kupitia mitandao ya kijamii kwa haraka kadiri zinavyojitokeza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!