Latest Posts

USITISHAJI MAPIGANO WAVUNJIKA DRC, M23 WAPAMBANA NA WANAMGAMBO ‘WANAOSAPOTIWA’ NA SERIKALI

Mapigano mapya yameibuka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali, hali ambayo imevunja makubaliano ya usitishwaji mapigano yaliyokuwa yamedumu kwa wiki kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Habari la DW, mapigano hayo yalianza alfajiri ya siku ya Jumapili, na kusababisha majeruhi 14, wakiwemo vijana wawili.

Makubaliano ya usitishaji mapigano kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23, wanaodaiwa kupata msaada kutoka Rwanda, yalifikiwa mapema mwezi Agosti baada ya upatanishi wa Angola.

Hata hivyo, mazungumzo ya amani kati ya Kinshasa na Kigali yamekwama, ingawa duru mpya ya mazungumzo imepangwa kufanyika mwishoni mwa wiki ijayo mjini Luanda, Angola.

Mgogoro huu unazidi kuchochewa na madai ya Rwanda kuwa kundi la Wahutu wenye msimamo mkali, FDLR, linaloendesha shughuli zake eneo hilo, linatishia usalama wa taifa hilo. Tangu waasi wa M23 walipoanzisha tena mashambulizi mwishoni mwa mwaka 2021, wameweza kuteka maeneo makubwa mashariki mwa Kongo, eneo ambalo lina utajiri wa madini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!