Latest Posts

HOSPITALI YA RUFAA MBEYA YAPATA MASHINE ZA KISASA KWA JUHUDI ZA MARAFIKI WA HOSPITALI

Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson, amekabidhiwa vifaa mbalimbali vya upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya vilivyonunuliwa na marafiki wa hospitali hiyo kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 100.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Dkt. Tulia ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, amewapongeza wadau hao wa maendeleo akisema wamekuwa wakifanya mambo ya muhimu kwa kukusanya michango na kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji kwa wanawake ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu ya huduma za kiafya.

Aidha Tulia amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi anayoendelea kufanya, na kuhakikisha wanawake wanapewa kipaumbele zaidi kwenye matibabu nchini akisema kwa dhamira hiyo ya Dkt. Samia ni wazi kwamba mwakani wanakwenda kumchagua kwa kishindo kuwa Rais kwa kipindi cha pili.

Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, Jumanne Masea, ametoa shukrani kwa marafiki wa hospitali hiyo kwa msaada wao, ikiwemo ununuzi wa mashine za usingizi ambazo ni muhimu katika upasuaji. Amesema msaada huo utaimarisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Mbeya, Oliva Kibona, amesema juhudi za kuhamasisha wanawake na wadau wengine zilikuwa ngumu, lakini hatua hiyo imefanikiwa. Ameongeza kuwa Rais Samia ameendelea kuwasaidia wanawake kwa kiwango kikubwa kuhakikisha wanapata huduma bora katika mazingira mazuri.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!