Latest Posts

MGOMBEA CHAMA CHA MAKINI: SAMIA ATABAKI SERIKALINI NIKISHINDA URAIS

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Makini, Coaster Jimmy Kibonde, amesema endapo atashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, atamwacha Rais wa sasa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndani ya serikali yake kwa nafasi maalumu ya kushughulikia diplomasia.

Kibonde, ambaye amezungumza kupitia kipindi cha Clouds360 cha Clouds TV, amesema amegundua Dkt. Samia ni mwanadiplomasia mahiri, hivyo atamkabidhi jukumu la kuongoza dawati maalumu litakalokuwa na idara tatu zinazoshughulika na masuala ya kisiasa, kiuchumi na ya kimataifa.

 

“Nimesema nikishinda urais, Mama Samia nitamwacha Ikulu. Nimegundua Mama Samia ni mwanadiplomasia mzuri mno. Kwenye diplomasia ya kisiasa, kiuchumi na mambo ya nje yuko vizuri. Kwa hiyo atakuwa mkuu wa dawati maalumu katika serikali yangu. Asiwe na presha, ajira nimeshamuahidi,” amesema Kibonde.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!