Latest Posts

TEA YAJADILI UTEKELEZAJI WA SHUGHULI NA MPANGO KAZI MPYA KUPITIA BARAZA LA WAFANYAKAZI

 

Kaimu Mkurugenzi Utafutataji Rasilimali na Usimamizi Miradi ya Elimu Bw. Masozi Nyirenda akitoa ufanunuzi kuhusu utekelezaji wa miradi ya elimu kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA mjini Morogoro.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA Dkt. Erasmus Kipesha akisisitiza jambo katika kikao cha tano kilichofanyika mjini Morogoro Septemba 11 na 12, 2025. Kulia ni Katibu msaidizi Bw. Lusungu Kaduma.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA Bi. Mwanaisha Komba akitoa maelezo kwa wajumbe wa baraza hilo katika kikao cha tano kilichofanyika mjini Morogoro kwa lengo la kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji na kiutumishi.

Wajumbe wa Baraza la Pili la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana kwenye kikao cha tano cha baraza hilo Morogoro.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA Dkt. Erasmus Kipesha (kulia) pamoja na Katibu wa Baraza hilo Bi. Mwanaisha Komba (kushoto) wakifuatilia taarifa na maoni kutoka kwa wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha tano kilichofanyika Morogoro.
Kaimu Meneja Usimamizi wa Miradi ya Elimu Bi. Mwafatma Mohamed akijibu maswali ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA walipokutana mjini Morogoro kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani CPA. Richard Mazinge akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA kwenye kikao cha tano kilichofanyika mjini Morogoro kwa lengo la kupitia na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji za mamlaka. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi CPA.Mwanahamis Chambega

Morogoro –

Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamekutana kwa siku mbili mkoani Morogoro katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kujadili utekelezaji wa shughuli za Mamlaka kwa mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na kuwasilisha na kuchambua mpango kazi wa mwaka 2025/2026.

Kikao hicho cha siku mbili kilichoanza Septemba 11 hadi 12, 2025 kimeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha.

Katika kikao hicho, wajumbe walipata fursa ya kupokea taarifa za utekelezaji kutoka kwa vitengo mbalimbali vya Mamlaka, na kutoa maoni na mapendekezo ya namna ya kuboresha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi zaidi.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, Dkt. Kipesha alieleza kuwa Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu linalowawezesha watumishi kushiriki moja kwa moja katika upangaji wa mipango na utekelezaji wa majukumu ya taasisi.

Alisisitiza kuwa ushiriki wa watumishi katika kujadili utekelezaji wa majukumu ya mamlaka na mikakati iliyowekwa kwenye utekelezaji ni msingi wa uwajibikaji, ufanisi na mafanikio ya taasisi kwa ujumla.

“Mkutano huu ni fursa mahsusi ya kujitathmini, kubadilishana mawazo, na kupanga kwa pamoja mikakati ya kuimarisha utendaji wetu ili kufanikisha malengo ya Mamlaka,” alisema Dkt. Kipesha.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!