Latest Posts

AJALI YA MAJI NJOMBE: MAMA AJITOSA KUOKOA WATOTO, AFARIKI PAMOJA NAO

Watu watatu, wakiwemo watoto wawili wa mfanyakazi wa benki ya NMB, wamefariki dunia baada ya kuzama katika maporomoko ya maji yaliyopo Hifadhi ya Mpanga Kipengere, mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililojiri Septemba 14, 2025 majira ya saa nane na nusu mchana, wakati wa sherehe ya pamoja (get together) ya wafanyakazi wa NMB kutoka matawi ya Makambako, Wanging’ombe na Makete.

Waliofariki wametajwa kuwa ni Michelle Mwasongwe (5) na Jannel Mwasongwe (4), watoto wa mfanyakazi wa NMB tawi la Makambako, Bertha Nicodem, pamoja na Lilian Mandali (31).

Taarifa zinaeleza kuwa watoto hao walianza kuogelea lakini wakashindwa kuyamudu maji, na ndipo Lilian Mandali alipojitosa kujaribu kuwaokoa, lakini naye alizama na kufariki dunia.

Miili ya marehemu hao imeopolewa na kuhifadhiwa katika Kituo cha Afya cha Mbuyuni wilayani Mbarali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!