Ripoti mpya ya shirika la kikanda linaloundwa na nchi za Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika IGAD (Intergovernmental Authority on Development) imesema watu milioni 42 wanakabiliwa na kiwango kikubwa cha uhaba wa chakula mwaka huu.
‎Ripoti hiyo imetolewa Shirika hilo Septemba 16, 2025 huku ikizitaja nchi wanachama ikiwemo Djibouti, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda kuathirika zaidi.
‎Kulingana na uchunguzi wa IGAD ambao umefanyika tangu mwaka 2016, idadi ya watu wanaokabiliwa na upungufu wa chakula imeongezeka mara tatu katika nchi za hizo huku shirika hilo lilisema kwamba idadi ya watu walio kwenye uhitaji mkubwa wa chakula iliongezeka kutoka milioni 13 mwaka 2016 na kupindukia zaidi ya milioni 40.
‎Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Taifa la Sudan linaoongoza kukabiliwa na uhaba wa chakula ambapo zaidi ya watu milioni 24 wapo katika nyangati ngumu za upataji chakula ikichochewa zaidi na mgogoro unaoendelea nchini humo.
‎Taarifa imebainisha kwamba kutokana na upungufu mkubwa wa msaada hasa katika chakula umesababisha utapiamlo kuongezeka zaidi kwenye eneo lote la ukanda hasa kwa watoto wadogo.
‎Aidha mabadiliko ya katiba nchi yameainishwa kama moja ya sababu kuu inayopelekea kupungua kwa uzalishaji wa chakula katika mataifa hayo, ambapo ili kufia utatuzi mipango maalumu imetakiwa kuanzishwa ikiwa ni pamoja na uongezaji wa misaada ya chakula ili kuwanusuru wakazi wa maeneo hayo.