Latest Posts

TAMESOT YAIPONGEZA POLISI KAGERA KWA KUBAINI UKWELI WA MAUAJI YA SHADIDA

Chama cha Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania (TAMESOT) kimelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na madaktari wa Kituo cha Afya Bunazi kufanya uchunguzi wa kina uliobaini ukweli wa mauaji ya kikatili ya Shadida Shamsi, aliyekuwa mkazi wa Kitongoji cha Omkitwe, Wilaya ya Misenyi.

Katibu Mkuu wa TAMESOT, Bw. Lukas Joseph Mlipu, akizungumza akiwa Kibaigwa, Dodoma, amesema awali tukio hilo lilisababisha taharuki kubwa baada ya uvumi kuenea kwamba marehemu aliuawa kwa imani za kishirikina na kuondolewa baadhi ya viungo vya mwili.

Hata hivyo, taarifa ya uchunguzi iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda, imebainisha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi. Inadaiwa Shadida aliuawa na mtu anayedhaniwa kuwa mpenzi wake baada ya kumfuata nyumbani kwake na kumchinja shingo kwa kitu chenye ncha kali kisha kumchoma tumboni, bila kuondolewa kwa viungo kama ilivyoripotiwa awali.

Mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa familia yake Septemba 17, 2025 na kuzikwa katika Kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Nyankele, Kata ya Mabale, Wilaya ya Misenyi, huku juhudi za kumsaka mtuhumiwa zikiendelea baada ya kutoweka mara baada ya tukio hilo Septemba 16.

 

Bw. Mlipu amewataka wananchi kuwa makini wanapotoa taarifa za matukio mazito kama mauaji ili kuepusha taharuki na kuichafua jamii kwa uvumi usio na msingi. Aidha, ametoa rai kwa waganga wa tiba asili na tiba mbadala kuhakikisha huduma wanazotoa zinafuata maadili, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!