Latest Posts

MBETO: ACT KINA SERA HATARI ZA UKABILA NA UBAGUZI

Chama Cha Mapinduzi kimesema ACT Wazalendo kina   ajenda ya siri na sera za ubaguzi hivyo ni hatari kwa mustakabali wa amani ya Zanzibar na watu wake ikiwa siku moja kitachaguliwa na wananchi.

Kimeitaja  hatua ya Makamu   Mwenyekiti wake Ismail  Jussa Ladhu,  kumshambulia mgombea Urais  wa CCM , Rais Dk  Hussein Ali Mwinyi  akidai  hana asili ya Zanzibar ni ushahidi  tosha ACT si chama sahihi.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum  ya NEC  Zanzibar ,  Idara ya Itikadi  , Uenezi na Mafunzo , Khamis Mbeto  Khamis , aliyesema  ACT kina Sera za  kibaguzi na ubaguzi  ni hatari  kwa ustawi  wa Umoja na Mshikamano.

Mbeto alisema karibu wananchi wote wa Zanzibar ,aidha watakuwa na Asili moja  ya Zanzibar na nchi nyingine,   hivyo ACT kusema kikishinda wasio na  Asili ya Zanzibar  watarudishwa kwenye  Asili zao  huo ni ubaguzi mpya.

Akitoa mfano alisema kwa Zanzibar  utawaondoa watu wangapi na kuwaacha wangapi, kwani  kulingana na  jiografia ya Zanzibar  ni mkusanyiko wa Asili za watu,makabila na rangi  wa mbalimbali   duniani.

“Jussa amekuwa akimnyooshea kidole  Rais Dk Mwinyi na kudai ana asili ya Mkuranga Tanzania Bara. Cha ajabu  Jussa  hataji  Asili yake ni India. Mtu mwenye Asili ya Mkuranga na India yupi aliyetoka nje ya Bara la Afrika? ‘Alihoji Mbeto

Aidha  , Katibu  huyo  Mwenezi  alisema katika dunia ya sasa ambayo muafrika amezaa na Mjapani, kuna  Wachina na magoa   waliozaliwa Zanzibar , na mtu  mwenye  asili ya Rwanda na Malawi  amekuwa Rais wa Kwanza  Zanzibar, madai ya Jussa ni zaidi ya  upuuzi.

“Zama ya Ubaguzi wa rangi ,Asili na ukabila imekwisha duniani. Kiongozi anayebagua wenzake  kwa Rangi, Kabila  au Asili   ni katili kuliko  kiongozi wa zamani Afrika  Kusini Pick Botter ” Alieleza

Mbeto  akimshutumu vikali Jussa , huku akimwita  Mwanasiasa  mapepe,  anayeshindwa  kujenga hoja za kisiasa na  kuwa  mfuasi wa  Sera za jikoni zenye mipasho ya  unyago na kidumbaki.

‘Hutamsikia hata siku moja akinadi sera za chama chake jukwaani . Anachokijua  ni mtamko ya ubaguzi, wivu wa wake wenzake na chuki binafsi “Alisema Katibu huyo Mwenezi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!