Latest Posts

MRAJISI MSAIDIZI AITAKA CBT KUWASIMAMIA WANUNUZI KULIPA MALIPO YA KOROSHO KWA WAKATI

Mrajisi Msaidizi wa Vyama Vikuu vya Ushirika Muhamed Lilanga ameiomba Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kuwasimamia wanunuzi wa zao la korosho kulipa malipo kwa wakati kwa sababu wanunuzi wako chini ya bodi.

Ametoa wito huo kwenye mnada wa tano wa zao la korosho wa Chama Kikuu cha Ushirika MAMCU kinachohudumia wilaya ya Nanyumbu, Masasi na Mtwara, uliofanyika Halmashauri ya Mji Masasi.

Amesema wanaochelewesha malipo si vyama vya ushirika, ila wapo baadhi ya wanunuzi wamekuwa wakichelewesha malipo  na lawama kuwaangukia vyama vya ushirika hivyo ameiomba bodi kuwasimamia wanunuzi kulipa malipo kwa wakati.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika MAMCU, Alhaji Azam Mfaume, amesema wameingiza tani 10,000 daraja la kwanza  wameuza tani zaidi ya 8,000 kwa bei ya juu shilingi 2,550 na bei ya chini shilingi 2,110; na daraja la pili ni zaidi ya tani 2,000 kwa bei ya juu shilingi 2,260 na chini shilingi 1,860.

Na kuongeza kuwa changamoto ndogondogo zinazojitokeza ni wakulima kutokulipwa kwa wakati, ambapo wakulima wenyewe wanategemea kulipwa fedha kwa wakati mara baada ya kuuza mazao yao.

Hivyo amewaomba wawakilishi wa wanunuzi wa korosho waliopo nchini kuzingatia kulipa kwa wakati, ili iwarahisishie na wao kufikisha fedha kwa wakulima kwa wakati.

Glory Kennedy kutoka Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) amesema toka kuanza kwa minada wamepeleka sokoni jumla ya tani 370,000 zenye thamani ya shilingi trilioni moja na kuwaasa wakulima kuendelea kuzingatia ubora wa korosho ili kulinda thamani ya bei ya zao hilo

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!