Zaidi ya vijana 160 wanaojishughulisha na kilimo katika Wilaya ya Makete Mkoani Njombe wamepewa mbolea bure na serikali Wilayani humo ili kuwapunguzia mzigo katika msimu huu wa kilimo.
Anilea Sanga na Yusuph Tweve ni miongoni mwa vijana wilayani humo waliofanikia kukabidhiwa mbole ambao wanasema walifikisha ombi la kusaidiwa mbolea kwa Mkuu wa wilaya hiyo Kissa Kasongwa kutokana na changamoto ya upatikanaji kwenye maeneo yao ya kilimo.

Akizungumza baada ya kukabidhi Mbolea DC Kissa amesema alipokutana na baadhi ya vijana walitoa ombi hilo ambapo kwa kushirikiana na baadhi ya wadau wa kilimo wakiwemo wafanyabiashara wa pembejeo,TFC pamoja na TFRA wameweza kuanza na vijana 160 kati ya walengwa zaidi ya 1500 ambapo Mbolea mifuko 290 yenye thamani ya zaidi ya Milioni ishirini na moja ikitolewa kwa vijana hao.

“Vijana waliniambia tunahitaji kusukumwa kidogo lakini tunachokosa ni mbolea kwa hiyo ninaamini shughuli ya leo inaenda kuacha tabasamu kwa vijana, na ambao kweli watachukua mbolea hii na kwenda kupeleka kwenye kilimo tunaamini mwakani tutakuwa tunaongea mengine”amesema DC Kissa