Latest Posts

RAS MORO: BIMA YA AFYA KWA WOTE YAHITAJI HUDUMA BORA NA UADILIFU

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa, amewataka watumishi wa sekta ya afya na sekta nyingine mkoani humo kuacha tabia ya ubabaishaji na kutoa huduma kwa weledi, uwajibikaji na uadilifu kwa wananchi.

Dkt. Mussa ametoa agizo hilo wakati akifungua mafunzo ya utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote yaliyowakutanisha Waganga Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Wilaya pamoja na Wakuu wa Vituo vya Afya kutoka mkoa mzima wa Morogoro.

Amesisitiza kuwa watumishi wa umma, hasa wale waliopo katika kada ya afya, wana jukumu kubwa la kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa kila mwananchi bila upendeleo wala rushwa, akisema hatua hiyo ni muhimu katika kufanikisha azma ya Serikali ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya kwa uhakika.

Ameongeza kwa kusema kuwa Bima ya Afya kwa Wote ni moja ya ajenda ya vipaumbele vya Serikali ndani ya siku 100 za utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi, hivyo ni lazima kila mtumishi ahakikishe anashiriki kikamilifu kuelimisha na kusimamia utekelezaji wake

Kwa upande wake, Dkt. Irene Haule kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu– TAMISEMI, amesema Serikali imeanza utambuzi wa watu wasio na uwezo ili waweze kupatiwa bima ya afya kwa msaada wa Serikali, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha hakuna mwananchi anayekosa huduma ya afya kwa sababu ya hali ya kiuchumi.

Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameahidi kwenda kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na bima ya afya, huku wakiahidi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha mkakati huo wa Serikali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!