Latest Posts

BARAZA LA MADIWANI MTWARA MIKINDANI LATAKA HATUA ZA HARAKA KUBORESHA BARABARA

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani limeitaka menejimenti ya manispaa hiyo kuchukua hatua za haraka kuboresha miundombinu ya barabara katika kata mbalimbali, kufuatia changamoto zinazoendelea kujitokeza hususan katika kipindi cha mvua.

Maelekezo hayo yametolewa Leo Januari 29,2026 kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kupitia taarifa za kata, ambapo madiwani waliwasilisha hali halisi ya miundombinu katika maeneo yao.

Diwani wa Kata ya Chuno, Mariamu Chimbwai, amesema baadhi ya barabara katika kata hiyo zimekuwa hazipitiki kutokana na mifereji kuziba, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Likombe Saidi Salumu, amesema kutotekelezwa kwa uchongaji wa barabara kwa mwaka 2025 kumesababisha uharibifu mkubwa wa barabara nyingi katika kata hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Naibu Meya Sixmund Lungu amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya manispaa na TARURA ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za barabara, sambamba na mpango wa kusogeza huduma za serikali karibu na wananchi kwa kujenga ofisi za serikali za mitaa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!