Latest Posts

KAMATI YA SIASA CHAMWINO YARIDHISHWA NA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA MIJI 28

Leo Februari 10, 2026, Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Chamwino ikiongozwa na Mwenyekiti wake amabaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Janeth Mayanja imefanya Ziara ya Kutembelea Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA).

Mhe. Mayanja amesema Kamati ya Siasa imeridhishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao utaenda kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Chamwino, hasa katika maeneo yenye mgao wa maji, ikiwemo Kata ya Chamwino, Msanga na Buigiri.

Amesema, wananchi wa Wilaya ya Chamwino wanamshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya katika Wilaya ya Chamwino.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chamwino, Mhe. George Malima, ameipongeza Wizara ya Maji na DUWASA kwa kusimamia mradi huo na kuomba Mkandarasi kukamilisha kwa wakati mradi huo.

Akisoma taarifa ya mradi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Meneja wa DUWASA Kanda ya Chamwino, Mha. Gray Mbalikila, amesema lengo la mradi huo ni kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi katika Mji wa Chamwino, ambapo kukamilika kwake  kutachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja kupunguza magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji.

Amesema gharama za mradi huo ni Shilingi Bilioni 17 ambazo zinahusisha uchimbaji wa visima virefu vinane ambavyo vimekamilika, ujenzi wa tenki la kuvunia maji la lita laki tano na miundombinu ya kusukuma na kutibu maji katika eneo la Chamwino.

Kazi nyingine zinazofanyika katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa tenki la laki mbili katika eneo la Msanga na uchimbaji na ulazaji wa Bomba za kipenyo kikubwa cha Inchi 6 hadi 16 kwa umbali wa kilometa 47.

Mradi umefikia asilimia 68 ya utekelezaji wake ambapo mkataba wa mradi huu ulisainiwa tarehe 6 Juni, 2022 na utekelezaji wake ulianza mwaka 2023 na unatarajiwa kukamilika tarehe 10 Agosti, 2026, huku Mkandarasi amepewa maelekezo na Katibu Mkuu, Wizara ya Maji kuhakikisha ifikapo tarehe 31 Machi, 2026 awe ameanza kufanya majaribio ya Mradi.

Kukamilika kwa Mradi huo utaongeza upatikanaji wa Majisafi kutoka asilimia 91 ya sasa hadi asilimia 100 na utaenda kuhudumia wananchi zaidi ya 59,085 katika eneo la kihuduma la DUWASA katika Mji wa Chamwino, ambapo Kata 4 zenye jumla ya Vijiji na Mitaa 7 na Vitongoji 48 watanufaika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!