Latest Posts

SERIKALI KUIMARISHA SEKTA YA KINGA YA JAMII, KULETA MANUFAA KWA UMMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete amesema Serikaili ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuimarisha sekta ya kinga ya jamii ili kuleta manufaa kwa umma.

“Rais anatamani na amedhamiria kwa dhati kuongeza wigo wa wananchi wanaopata huduma za kinga ya jamii hasa wale waliojiajiri katika sekta isiyorasmi, hivyo ninaimani kuanza kutumika kwa Sera Mpya ya Kinga ya  Jamii ya mwaka 2023 itawanufaisha wananchi” alisema Mhe. Kikwete.

Ameyasema hayo Februari 10, 2026 wakati akizungumza na kufunga Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii uliofanyika katika Ukumbi wa AICC- Jijini Arusha.

Ameongeza kuwa, dhimira hii ya Rais imesababisha kutungwa kwa Sera ya Kinga ya Jamii ya mwaka 2023 na  imezinduliwa rasmi tarehe 9 Fesbruari 2026. Sera  hiyo inalenga kuhimiza wananchi wote wenye uwezo wa kuzalisha kipato wananjiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii. Lengo la mwelekezo ili  kila mtanzania anufaike na huduma za Kinga ya Jamii kwa uchangiaji  zinazotolewa na NHIF, PSSSF na NSSF.

Aidha, alifafanua kuwa, Kinga ya Jamii ni uwezeshaji wananchi kupitia michango inayotolewa kwa njia mbili  ambazo ni watumishi  wa umma na wa sekta binafsi wanaopata mshahara kuchanga wenyewe na wananchi wasiojiweza mathalani wazee, akina mama na watoto kusaidiwa kwa kuchangiwa na Serikali kupitia mifuko na programu mbalimbali.

“Sisi Tanzania ni moja kati ya nchi 17 Barani Afrika ambazo zimefanikiwa kutekeleza eneo la kinga ya jamii kwa kuwezesha wananchi kupitia michango inayotolewa na watumishi wa umma au watumishi walio katika sekta binafsi na wale wasio na uwezo wanachangiwa na Serikali” alisema Mhe. Kikwete

Mhe. Kikwete alisisitiza kuwa, Tanzania ina kila sababu ya kujivunia jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao unawasaidia wananchi kuinuka kiuchumi, hvyo kuifanya Tanzania moja ya nchi barani afrika zinazowafikia wananchi wengi katika sekta isiyorasmi.

Vile vile, aliwashukuru na kuipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano kwa kuandaa mkutano wa wadau wa Sekta yak inga ya jamii na kuimarisha mazingira wezeshi ya utekelezaji wa sekta ya Kinga ya Jamii ambayo itainua maisha ya watanzania walio wengi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!