Latest Posts

MILIONI 80 ZATENGWA KUJENGA VIZIMBA VYA KUDHIBITI MAMBA NYASA

Katika kuimarisha usalama wa wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao kandokando ya Ziwa Nyasa, Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imetenga jumla ya shilingi milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa vizimba viwili vya kudhibiti mamba katika vijiji vya Kihagara na Mtipwili.

Fedha hizo zilikabidhiwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Peres Magiri, kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mhe. Khalid Khalif kwa lengo la kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi ambapo kila kizimba kitagharimu shilingi milioni 40, hivyo kufanya jumla ya shilingi milioni 80 kwa vizimba vyote viwili.

Mradi huo unatekelezwa ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa ziara yake ya kampeni wilayani humo.

Ujenzi wa vizimba hivyo unalenga kupunguza matukio ya mashambulizi ya mamba kwa wananchi, hususan katika maeneo ya mwalo hivyo hatua hiyo inatarajiwa kuongeza usalama kwa wavuvi pamoja na kina mama wanaofanya shughuli mbalimbali za maendeleo pembezoni mwa ziwa, na hivyo kuweka mazingira salama kwa shughuli za kila siku za kijamii na kiuchumi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!