Latest Posts

HATIMILIKI ZAZIDI KUIMARISHA USALAMA WA ARDHI GEITA

Zaidi ya wananchi 116 wa Kijiji cha Nyakagwe kata ya Butolewa wameishukuru Serikali kwa kupanga kupima na kutoa hati miliki za ardhi, zoezi lililofanywa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Kampuni ya Settlement Solution iliyohusika na shughuli za upimaji.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la urasimishaji makazi, Mratibu wa Urasimishaji Makazi kutoka Kampuni ya Settlement Solution, Witness Jonathan, amesema kuwa tayari viwanja 1,320 vimepimwa na vina sifa ya kupatiwa hati miliki.

 

Naye Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Geita Region, Palmon Martin, amesisitiza umuhimu wa wananchi kumiliki hati za ardhi, akieleza kuwa hati huongeza thamani ya mali na kuwezesha upatikanaji wa mikopo katika taasisi za kifedha.

 

Baadhi ya wananchi na viongozi wa kata waliopatiwa hati wameishukuru Serikali kwa kuanzisha punguzo la gharama za upimaji na kurahisisha mchakato wa upatikanaji wa hati miliki.

Kwa ujumla, zoezi hilo limeelezwa kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha usalama wa makazi, kupunguza migogoro ya ardhi na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!