Ushahidi katika kesi ya uhaini ya Mwanasiasa Tundu Lissu umeendelea leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ambapo shahidi wa kwanza anaelindwa P2 (38) Mkristo, Mkazi wa Makarawe, Songea ambae ni fundi umeme ameshatoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Igras Mwinuka.
Ameieleza mahakama kuwa yeye ni mfuasi wa CHADEMA kuanzia 2021 na alianza kujishughulisha kwenye mikutano na michango ya mikutano tonetone.
Anaeleza kuwa tarehe 4/4/2025 alikuwa kwenye shughuli zake Songea anakumbuka kipindi anapitia mtandao wa kijamii alikutana na video ya LISSU ambapo alikuwa na mkutano Dar es Salaam
Akiwa kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube wakati anaperuzi akakutana na ujumbe wa Mwenyekiti wa chama akiwalekeza kuwa Mwaka huu (mwaka jana) hakutakuwa na uchaguzi kwa wale ambao wanataka kugombea udiwani, ubunge na Urais wasahau

Anaeleza kuwa Lissu lielekeza namna ya kuzuia uchaguzi usifanyike ili kupata mabadiliko. Baada ya ujumbe huo akapata hamasa ya kupata ufafanuzi zaidi wa namna ambavyo jambo hilo litafanyika akaanza kutafuta viongozi walio Songea ili kujua jambo hilo litafanyika vipi.
Akamtafuta Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Essau Siza ili kupata ufafanuzi anasema ilipofika tarehe 7/4/2025 akatafutwa na kuambiwa kuna ziara ya Lissu itafanyika mkoa wa Ruvuma watoe mchango wa hiyari tone tone ambapo yeye akatoa 10,000 ili kuwezesha ziara.
Anaeleza waliambiwa mkutano utafanyika tarehe 10/4/2025 saa nne asubuhi akaendelea na shughuli zake akisubiri hiyo siku. Ilipofika Tarehe 9/4/2025 akifuatilia taarifa za habari kwenye mitandao ya kijamii akapata taarifa za kuwa Lissu amekamatwa anadai hakuwa na taarifa za kutosha ilipofika tarehe 10/4/2025 akajiandaa kwenda kwenye mkutano kupata taarifa zaidi.
Alipofika uwanjani akakuta magari ya polisi akakuta taarifa za kuwa hakutakuwa na mkutano ndipo akatoka kwenda mjini kwenye ofisi za CHADEMA eneo la Mfaranyaki mchana. Wanachama wengine wa CHADEMA wakawa wanasema Heche ataongea akawa anasibiri kupata ufafanuzi kwa nini mkutano haujfanyika na kwa nini Mwenyekiti amekamatwa.
Kipindi anaelekea huko alipofika akakuta viongozi wa mkoa Heche, Lema na wengine kabla hawajaongea na waandishi yakaja magari ya polisi na kuwaambia wapo chini ya ulinzi akajikuta amekamatwa na kupelekwa Polsi kwa RPC.
KITUO CHA POLISI
Anasema alipofika aliwekwa mahabusu baada ya kuhojiwa akaambiwa anatuhumiwa kwa uchochezi na kufanya vurugu baada ya kutoa maelezo akaachiwa kwa dhamana akatakiwa kuripoti kila jumatatu. Ambapo aliripoti tarehe 14/4/2025, na tarehe 21/04/2025 ambapo ilikuwa siku kuu ya pasaka hivyo akaenda kuripoti 22/4/2025.
Anasema askari aliyekuwa anaenda kuripoti kwake akamchukua na kumpeleka Central kuchukuliwa maelezo yake tena kwa mara ya pili. Alipofika kwa huyo Kamanda akaambiwa aeleze anachokifahamu mwanzo mwisho kilichopelekea yeye kukamatwa kuanzia tarehe 10/4/2025 na anavyojishughulisha kwenye shughuli za chama.
Akachukuliwa maelezo mengine na Afande Juma akaeleza anamfahamu Lissu kama mwanasiasa maarufu kupitia mchango wake bungeni, alipokuwa Makamu Mwenyekiti na kugombea Uenyekiti.
ALIPOULIZWA JUU YA KUZIUIA UCHAGUZI
Anasema alikuwa hajui uchaguzi utazuiwa vipi lakini Mwenyekiti alisema wataenda kufanya uasi kuhamasisha mabadiliko ambao wangekua pamoja nae wangeenda nae. Alieleza tena kuwa alikuwa hajui namna gani wangezuia uchaguzi.
Hapa akawa ametamatisha ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Ignas Mwinuka.