Latest Posts

SHAHIDI MTATA ‘MWANACHADEMA’ ALIYEMKATAA LISSU AKERWA NA MASWALI ASEMA ‘YA KITOTO’

Baada ya shahidi P8 kumaliza kutoa ushahidi wake Lissu alipewa nafasi ya kuuliza maswali ya dodoso(cross examination)

 

Lissu: Ukionyeshwa maelezo yako uliyoandika utayatambua

Shahidi: Sio jukumu langu ni la mawakili

Lissu: Unabishana na Mwenyekiti wako?

Shahidi: Sasa hivi wewe si Mwenyekiti ni mshtakiwa.

Lissu: Umesema 22/04/2025 ulipoenda kuripoti kwa RCO ulichukuliwa na afande akakupeleka kwenye ofisi ya afande mwingine Michael tuonyeshe kama kuna sehemu umeandika hayo.

Shahidi: hakuna sehemu kama hiyo

Lissu: Haya yote nimekuuliza na hayapo kwenye maelezo uliyoandika umesema mahakamani kwa sababu unaamini yana maanakweli au si kweli.

Shahidi: kweli

Lissu: Nitakosea nikisema kwamba hukusema polisi kwa sababu unaamini sio mambo muhimu

Shahidi: Utakosea

Lissu: Waeleze majaji kama umeeleza kwa nini hayo mambo hukuyasema 22/4/2025

Shahidi: Hapana

Lissu: Umesema Mwenyekiti alisema tutakinukisha Waeleze majaji kama katika hayo uliyoyasikia akisema tutakinukisha alieleza maana ya tutakinukisha

Shahidi: Uliieleza

Lissu: Nilisema ni nini

Shahidi: Kukinukisha ni kama tunafanya uasi

Lissu: Unafahamu maana ya kukinukisha kwa kiswahili

Shahidi: Ni hivo kukinukisha

Lissu: Inatokana na neno nuka au nukia

Shahidi: Mi nafahamu neno kukinukisha hayo mengine mi sielewi

Lissu: Waeleze majaji kama hiyo video uliyoiona mtandaoni umewasilisha leo mahakamani

Shahidi: Hapana

Lissu: Hasira zako ni kwa sababu ya wizi wa uchaguzi

Shahidi: Hayo najua moyoni mwangu twende kwenye point

Lissu: Waeleze majaji kama kuanzia tarehe 4/4/2025 Lissu ametoa kauli

Shahidi: Hajatoa kwa sababu ni mhalifu

Lissu: Ngoja nukuweke sawa kwa sababu we ni mwanachama wangu huwezi ukanisumbua

Shahidi: Mimi sio mwanachama wako mshtakiwa

Lissu: Umenigeuka

Shahidi: Kwa sababu umeniingiza kwenye hatia sikutarajia hata siku moja nitakuja sehemu kama hii.

Lissu: Waeleze majaji tangu ulivyoandika maelezo haya 2025 uliwasiliana na Polisi mara ngapi

Shahidi: Juzi tarehe 14 nilipigiwa simu nikiwa nyumbani natakiwa kufika Dar es Salaam

Lissu: Waeleze majaji kama umetishiwa na Kiongozi wa CHADEMA, mwanachama mfuasi

Shahidi: Nakumbuka alisema mtu yeyote anaetoa ushahidi kwa Mwenyekiti wetu lazima tusalimiane nae

Lissu: Aliyekuwa anasema hayo maneno ni nani

Shahidi: Ni watu ni mwanaume haiwezekani kumtaja kwa ajili ya ulinzi wangu binafsi.

Lissu: Kuna kiongozi yeyote wa CHADEMA au mfuasi alietishia ndugu zako

Shahidi: Hakuna maana hawanijui

Lissu: Umesema ulivyokamatwa tarehe 8/4/2025 ulihojiwa Polisi

Shahidi: Sikuhijiwa polisi nilihojiwa kwenye ofisi ya RCO

Lissu: Huyu RCO ni Polisi au Bwanamifugo

Shahidi: Mbona una maswali ya kitoto aise

Lissu: Nitakosea kwamba nikisema umefutiwa kesi ili uwe shahidi kwenye kwsi hii

Shahidi: serikali achana nayo sikutegemea, niliongea ukweli na leo nimejikuta huku.

Baada ya maswali ya dodoso kuisha hapakuwa na maswali ya Re-examination kutoka kwa jamhuri hivyo waliomba shauri kuahirishwa kwani hapakuwa na shahidi mwingine aliyeandaliwa kwa leo.

Ombi hili lilikubaliwa japo Lissu alipinga akitaka Jamhuri waamrishwe na kuleta mahakamani shahidi ambaye yupo hapa jijini Dar es Salaam jambo. Jaji Dunstan Ndunguru alitoa amri kwa Jamhuri kuanzia kesho kuleta mashahidi kuanzia watatu na kuendelea.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!