Latest Posts

DC BUSEGA ATOA ONYO KWA WAKULIMA WASIOFUATA TARATIBU ZA KILIMO CHA PAMBA

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Faidha Salim, amewataka wakulima wa pamba kufuata taratibu na miongozo ya kilimo hicho, akisisitiza kuwa serikali haitatoa dawa za pamba kwa wakulima ambao hawatazingatia masharti yaliyowekwa.

Faidha ameyasema hayo Februari 21, 2026, wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto za wakulima katika vijiji vya Mwakiloba na Kijeleshi, Kata ya Mkula wilayani humo.

Alisema kuwa licha ya serikali kuwajali na kuwathamini wakulima, ni muhimu kuhakikisha wanazingatia utaratibu sahihi wa kilimo ili kulinda usalama wa mazao na afya za wananchi.

“Tunawaonea huruma wakulima na tunawapenda, lakini ni lazima wafuate utaratibu. Hatutatoa dawa za pamba kwa wakulima ambao hawajafuata taratibu, shamba lina mazao matano hapa tunatengeneza sumu kwenye mazao ya chakula,” amesema Mhe. Faidha.

Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya alitembelea mashamba ya wakulima na kujionea hali halisi ya kilimo cha pamba pamoja na changamoto zinazowakabili, huku akitoa elimu kwa wakulima ambao hawajazingatia kanuni za kilimo bora.

Amesema lengo la ziara hiyo ni kuwasaidia wakulima kuboresha uzalishaji wao kwa kufuata taratibu sahihi ili waweze kuwa wakulima bora zaidi katika msimu ujao wa kilimo cha pamba.

Aidha, amewahimiza wakulima kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa kilimo ili kuongeza tija, kulinda mazingira na kuhakikisha usalama wa mazao ya chakula pamoja na afya ya walaji.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!