Latest Posts

SOMALILAND YAISHAWISHI MAREKANI KWA MADINI NA KAMBI ZA KIJESHI; NI KATIKA KUSAKA UTAMBUZI WA KIMATAIFA.

Serikali ya Somaliland imetangaza kuwa iko tayari kuipa Marekani upendeleo maalum wa kupata madini yake adimu pamoja na fursa ya kujenga kambi za kijeshi katika ardhi yake.

Hatua hii inakuja wakati eneo hilo lililojitenga na Somalia tangu mwaka 1991 likizidisha harakati za kutafuta kutambulika rasmi kama taifa huru duniani.

Waziri wa Ofisi ya Rais wa Somaliland, Khadar Hussein Abdi, ameiambia AFP katika mahojiano yaliyofanyika Jumamosi kuwa wako tayari kutoa fursa za kipekee kwa Marekani ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kiulinzi.

“Tuko tayari kuwapa Marekani haki ya pekee ya kupata madini yetu. Pia, tuko tayari kutoa maeneo kwa ajili ya kambi za kijeshi. Tunaamini tutafikia mwafaka na Marekani,” alisema Bw. Abdi.

Somaliland imepata nguvu mpya baada ya Israel kuwa nchi ya kwanza duniani kuitambua rasmi uhuru wake mwezi Desemba 2025. Rais wa Somaliland, Abdirahman Mohamed Abdullahi, ameshaashiria kuwa Israel pia itapewa kipaumbele katika rasilimali za madini, na Waziri Abdi hakuondoa uwezekano wa kuruhusu Israel kuweka majeshi yake nchini humo.

Eneo la Somaliland liko mkabala na Yemen kupitia Ghuba ya Aden, eneo ambalo limekuwa na changamoto za kiusalama kutokana na mashambulizi ya waasi wa Houthi dhidi ya maslahi ya Israel na washirika wake.

Licha ya Somaliland kuwa na pasipoti yake, sarafu, jeshi, na polisi tangu mwaka 1991, Serikali ya Mogadishu (Somalia) bado inachukulia eneo hilo kama sehemu ya himaya yake. Hatua hizi mpya za Somaliland zinatarajiwa kuongeza joto la kidiplomasia kati ya Hargeisa na Mogadishu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!