Latest Posts

MAFUNDI NGUO GEITA WAPATIWA FURSA YA KUONGEZA UZALISHAJI

Tasnia ya ushonaji na ubunifu wa mavazi imeelezwa kuwa endapo itaboreshwa, inaweza kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi na kuongeza mapato ya fedha za kigeni yatokanayo na ubunifu wa mavazi.

Katika jitihada za kuinua tasnia hiyo, Equity Bank Tanzania tawi la Geita imekuja na mpango wa Ushonaji Plus wenye lengo la kuwawezesha mafundi cherehani wa viwango vya chini kwa kuwapatia mikopo ya mashine za kisasa za ushonaji wa nguo, hatua itakayoongeza uzalishaji na ubunifu katika shughuli zao.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwawezesha washona nguo yaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Afisa Uhusiano wa benki hiyo tawi la Geita, Alexender Tito, amesema wameanzisha mpango huo ili kuwasaidia mafundi kupata mashine za kisasa zitakazorahisisha kazi na kuongeza tija.

Kwa upande wake, Balozi wa Equity Bank Tanzania mkoani Geita, Bertha Komba, amesema mradi huo utasaidia kuboresha na kukuza sekta ya ubunifu wa mavazi mkoani humo, akibainisha kuwa bado mafundi wengi wanatumia mashine za zamani zinazopunguza kasi na ubora wa uzalishaji.

Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo ya mkopo wa mashine za ushonaji wameelezea manufaa watakayoyapata kupitia mpango huo, wakisema utaongeza uwezo wao wa kuzalisha nguo nyingi kwa muda mfupi na kuboresha kipato chao.

Mpango huo wa Equity Bank Tanzania unatarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko kwa mafundi ushonaji mkoani Geita, kwa kuongeza uzalishaji, ubora wa mavazi na kipato chao binafsi. Hatua hiyo pia inaelezwa kuwa sehemu ya mkakati mpana wa kuinua sekta ya ubunifu wa mavazi nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!