Latest Posts

WAKULIMA IRINGA WAPATIWA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UDUMAVU.

Katika jitihada za kupunguza tatizo la udumavu mkoani Iringa, wakulima kutoka vyama msingi vya ushirika vinavyosimamiwa na chama kikuu cha ushirika cha Iringa (IFCUM) wamepatiwa mafunzo ya kuzalisha viazi, mahindi, na maharagwe vyenye virutubisho mafunzo yaliyoambatana na ugawaji wa mbegu bure, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao yenye virutubisho na kuboresha lishe kwa watoto na kaya kwa ujumla.

Afisa mradi wa Harvest Plus mkoa wa Iringa, Mihambo Shija, amesema kuwa jitihada hizi zimepelekwa mkoa wa Iringa mahsusi kama sehemu ya mpango wa kupambana na tatizo la udumavu na utapiamlo.

Takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 zinaonyesha kiwango cha udumavu mkoani humo kilifikia asilimia 56.9. Hata hivyo, tafiti za hivi karibuni za mwaka 2023–2024 zinaonyesha kupungua kwa kiwango hicho hadi asilimia 30.1, jambo linaloashiria mafanikio ya hatua zinazochukuliwa sasa.

Nao baadhi ya wakulima waliohudhuria mafunzo hayo wakatoa ushuhuda wa jinsi elimu waliyopewa itakavyosaidia jamii hasa kuzalisha mazao yenye virutubisho na kuelimisha wengine kuhusu lishe bora kwa watoto na familia zao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!