Latest Posts

WANAFUNZI NYANKUMBU WAPATIWA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KUTOKA CRDB

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi imetoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu, ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto za hedhi wanapokuwa shuleni.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana amesema kuwa zawadi hiyo ina thamani ya shilingi milioni tano. Amesema pia benki hiyo ina mipango mbalimbali ya kuwawezesha wasichana na wanawake kufikia malengo yao ya kielimu na kiuchumi.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita Regina Mikenze, amewahimiza wanafunzi wenye vipaji katika shule hiyo kuwa na dhamira ya kuviendeleza ili vitakapowasaidia kufikia ndoto zao.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu Khadija Kayanda ameishukuru Benki ya CRDB kwa msaada huo, akisema utawasaidia wanafunzi wengi kuendelea na masomo yao kwa utulivu.

Sambamba na hilo, Benki ya CRDB pia imeshiriki kudhamini mashindano ya michezo mbalimbali shuleni hapo kwa kutoa mbuzi kama zawadi kwa washindi wa michezo ikiwemo mpira wa miguu na mpira wa pete, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha na kukuza vipaji vya wanafunzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!