Latest Posts

POLISI, UHAMIAJI, ZIMAMOTO NA TAKUKURU WAAHIDI USHIRIKIANO KWA I.PI.

Theophilida Felician, Kagera.

Vyombo za usalama mkoa Kagera viameahidi kutoa ushirikiano wakutosha kwa shirika linalojishughulisha na masuala ya utunzaji wa amani nchini INTERNATIONAL PEACE INFORMATION (IPI) katika masuala mbalimbali ikiwemo ya utoaji taarifa za uchunguzi kiusalama.

Vyombo hivyo vimetoa kauli hiyo mbele ya Rais wa shirika hilo Taifa Mh Prof Wilson George Munguza alipofika ofisi za mamlaka hizo kwa ajili ya kuwatambulisha  viongozi wa shirika mkoa Kagera na wilaya zake.

Utambulisho huo umefanyika ofisi za mamlaka  ya usalama mkoa ambazo ni jeshi la Polisi, Uhamijai, Zima moto na uokoaji sambamba  na Takukuru ambapo kila chombo kimepokea vyema ujio wa shirika hilo kutokana na malengo yake yakujikita kuisaidia serikali katika suala zima la utunzaji wa amani na mengineyo ya husuyo uchunguzi wa taarifa za usalama kwa kushirikiana na vyombo hivyo.

Hatahivyo wakuu wa Idara hizo wameahidi kuwa  ofisi zao zitajitolea  masuala kadhaa ikiwemo  suala la kutoa mafunzo ya  elimu kwa wana IPI ili kuwaongezea ujuzi  zaidi kwa lengo la kuwaweka sawa na kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Aidha Rais wa shirika  Prof Munguza amevipongeza na kuvishukuru vyombo hivyo kwa mapokezi mazuri ofisi zote ambapo amewahakikishia kazi ya kuisaidia serikali masuala ya uchunguzi na kuitunza amani yatafanyika kikamilifu maeneo mbalimbali ya nchi  kama ilivyokusudiwa na shirika hilo linalofanya kazi na nchi za Afrika mashariki na  makao makuu yake  yakiwa ni  mkoani Dare es salaam.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!