Latest Posts

WANAWAKE WAMI/RUVU WAONGOZA KAMPENI YA UHIFADHI WA MAZINGIRA MORO

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, wanawake wa Bodi ya Maji Bonde la Wami–Ruvu leo Machi 7, 2026 wameshiriki katika zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji cha Mto Mlali kilichopo mkoani Morogoro.

Katika zoezi hilo, zaidi ya miti 500 ikiwemo ya mikarafuu na michai ya chai imepandwa pembezoni mwa mto huo kwa lengo la kuimarisha kingo za mto, kuhifadhi mazingira pamoja na kulinda vyanzo vya maji.

Aidha, miti hiyo inatarajiwa kuwa fursa ya kiuchumi kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya jirani kwa kuwa baadhi ya mazao hayo yana thamani ya kibiashara ambayo inaweza kuwasaidia kuongeza kipato.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi wa Kufikia Dira ya Maendeleo 2050.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!