Bila uoga mkazi wa Makambako Wilayani Njombe anayefahamika kwa jina la Akida Tweve amejitokeza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka na kumuomba kutembelea mara kwa mara mji wa Makambako ili aweze kuona changamoto za mji huo.
Akieleza baadhi ya changamoto jana March 8 kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani kimkoa yaliyofanyika mjini Makambako baada ya wanaume kupewa nafasi ya kueleza Changamoto amesema.
“Kuna mtaa wanapika gongo lakini mimi nilienda kimya kimya juzi hapa nikawaonyesha Polisi wakakamata mpaka mashine,kwa hiyo Mtaka mimi nikuombe kuka muda mrefu bila kututembelea kuna vitu vingi vitakupita”amesema Akida
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameeleza kupokea ushauri wa wakazi wa Makambako huku pia akiagiza viongozi wa mkoa huo kufanyia kazi na kuto puuza jambo linalowakera wananchi.
