Latest Posts

MAAFISA UNUNUZI, UGAVI VETA WAJENGEWA UWEZO

Jumla ya Maafisa Ununuzi na Ugavi 120 kutoka Kanda zote za Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wanashiriki katika mafunzo elekezi jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo, hivyo kuimarisha utendaji kazi wao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi, VETA, Bi. Witness Mgimba amesema mafunzo hayo elekezi yameanza kutolewa tarehe 5 Machi, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha VETA Dodoma kwa kushirikiana na Maafisa Ununuzi wa VETA Makao Makuu, wataalam kutoka PPRA na wataalam kutoka Hazina, na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 12 Machi, 2026.

“mafunzo haya yanalenga kuimarisha utendaji kazi, kuhakikisha ufanisi, utunzaji wa mali za umma, matumizi ya mfumo wa Uhasibu Seriakalini (MUSE), kushirikisha makundi maalum katika ununuzi wa umma na kufuata taratibu za Serikali katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku,” amesema Bi Mgimba.

Sambamba na kupatiwa mafunzo hayo Bi Mgimba amesema watumishi hao watawasilisha changomoto  wanazokutana nazo katika utendaji kazi wao wa kila siku ili kwa umoja wao waze kuzipatia ufumbuzi.

 

Hata hivyo Bi mgimba amesema watumishi hao wanaendelea kupewa maelekezo katika eneo la usimamizi wa ugavi kutokana na maboresho yaliyofanyika katika Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2020/2023 ambayo inasisitiza utunzaji wa vifaa,vitendea kazi vinavyonunuliwa ili kutoisababishia Serikali hasara kwa kutokutunza vifaa hivyo au kuvifanyia matumizi yasiyokuwa sahihi.

Aidha Bi Mgimba ameishukuru Menejimenti ya VETA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu kwa kutoa kibali kwa maafisa hao kushiriki katika mafunzo  hayo.

Kwa upande wake Jacqline Sebastian,  Afisa Ununuzi Mwandazi kutoka MVTTC amesema amejifunza mambo mengi katika ununuzi wa umma ikiwa ni pamoja na kuhusisha Makundi Maalum kwenye ununuzi wa umma, ambapo makundi hayo yanajumuisha wanawake,vijana, wazee na watu wenye ulemavu.

 

Paul Mshabaha, Afisa Ununuzi kutoka Chuo cha VETA Iringa na mnufaika wa mafunzo hayo amesema, “Naishukuru VETA kwa kuandaa mafunzo haya hasa kwetu sisi ajira mpya, nimejifunza utunzaji wa mali za serikali,mfumo wa ulipaji Serikalini (MUSE), lakini tunatarajia kujifunza maadili ya utumishi umma ili tuweze kwenda kuwajibika kwa kufuata miongozo na taratibu za kiutumishi.”

 

VETA imekuwa ikitoa mafunzo elekezi kwa watumishi wa kada ya ununuzi na ugavi  ili kuelewa majukumu na kuwajenga uwezo ili kufikia malengo ya Serikali na kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!