Latest Posts

TEITI YATAKA WANANCHI WASHIRIKISHWE KATIKA MIRADI YA CSR

Mwenyekiti wa Tume ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini na Gesi (TEITI), Balozi Wilson Masilingi, amewasihi wadau wanaohusika na utoaji na utekelezaji wa miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kuwashirikisha wananchi kabla ya kuanza kutekeleza miradi katika maeneo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Geita, Masilingi amesema ni muhimu wananchi kupewa nafasi ya kushiriki katika kuchagua aina ya miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ili kuhakikisha inakidhi mahitaji halisi ya jamii.

Amesema ushirikishwaji wa wananchi utasaidia kuepusha utekelezaji wa miradi katika maeneo ambayo hayana uhitaji wa huduma au maendeleo hayo, hivyo kuhakikisha miradi ya CSR inaleta manufaa yaliyokusudiwa kwa jamii husika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!