Latest Posts

WANAWAKE KILOLO WAJENGEWA UWEZO WA UONGOZI KUONGEZA USHIRIKI KATIKA NAFASI ZA UAMUZI

Wanamtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wameendesha mafunzo ya uongozi kwa makundi ya wafugaji, vinara wa masuala ya jinsia, wanakamati wa vijiji pamoja na makundi ya wanawake wilayani Kilolo, yakilenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Mwezeshaji kutoka TGNP, Schola Makwaia, alieleza kuwa hapo awali mfumo dume uliwanyima wanawake nafasi na kipaumbele katika uongozi ndani ya serikali, taasisi, dini na hata katika umiliki wa ardhi, hali iliyochangia kudumaa kwa maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Iliongezwa pia baada ya kufanya tathmini, ilibainika kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu kwa jamii, kwani maendeleo endelevu yanahitaji ushiriki wa wanawake ili kufikia dira ya taifa ya mwaka 2050.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema wako tayari kutumia maarifa waliyopata kugombea nafasi za uongozi na kuwa mabalozi wa kuhamasisha wanawake wengine kujiamini na kushiriki kikamilifu katika nafasi za maamuzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!