Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, likiongozwa na Kamanda wa Polisi SACP Allan Bukumbi, limetoa onyo kali kwa watumiaji wa vyombo vya moto wanaoendesha wakiwa wamelewa pamoja na wahalifu wengine, kuacha vitendo hivyo mara moja, akisisitiza kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kufanya doria ili kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inaendelea kudumishwa.
Akizungumza na vyombo vya habari leo, Machi 20, 2026, Bukumbi ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kupambana na uhalifu na kusisitiza utayari wa jeshi hilo kuendelea kukabiliana na vitendo vya kihalifu.