Latest Posts

SENZIA: TUGHE KILIMANJARO KUTETEA MASLAHI YA WAFANYAKAZI

Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Mkoa wa Kilimanjaro wanatarajiwa kunufaika na uongozi mpya utakaolenga kuboresha ustawi wao, kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya chama na wadau wa maendeleo.

Matarajio hayo yanakuja baada ya Senzia Lushino kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa TUGHE Mkoa wa Kilimanjaro katika uchaguzi uliofanyika Julai 10,2026 wakati wa Mkutano Mkuu wa Mkoa, mjini Moshi ambapo alipata kura 48.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Afisa Kazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Elizabeth Kalenga, alisema nafasi ya uenyekiti iligombewa na wagombea watatu ambao ni Senzia Lushino, Peter Mashaka na Elisha Moses Mushi ambapo baada ya kura kupigwa, Peter Mashaka alipata kura 2 , huku Elisha Moses Mushi akipara kura sifuri na Senzia Lushino kushinda kwa kura 48.

Mbali na kumchagua mwenyekiti, wajumbe wa mkutano huo pia walichagua viongozi katika nafasi nyingine mbalimbali, zikiwemo Mjumbe wa Baraza, Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Wajumbe wa Kamati Tendaji, Mwakilishi wa Vijana, Mwakilishi wa Mahitaji Maalumu, Mwenyekiti wa Wanawake, Mweka Hazina wa Wanawake na Wajumbe wa Wanawake.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!