Latest Posts

RC MALIMA ATAKA MADIWANI KUJENGEWA UELEWA WA HOJA ZA CAG

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amewataka madiwani wa mkoa huo waliochaguliwa kuanzia Oktoba 29, 2025 kujengewa uwezo wa kutosha kuhusu majukumu yao ili waweze kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri zao.

Malima ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kilicholenga kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Amesema mafunzo hayo yatawawezesha madiwani kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu namna ya kufuatilia na kujadili hoja za CAG, kusimamia matumizi sahihi ya fedha za umma pamoja na kuhakikisha miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, shule na vituo vya afya inatekelezwa kwa viwango vinavyotarajiwa na kwa manufaa ya wananchi.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Stephen Kassaro, amesema ukaguzi unaofanywa na CAG unalenga kuimarisha uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za umma kupitia ushirikiano wa wadau wote,Amesisitiza kuwa halmashauri zinapaswa kushirikiana na wakaguzi tangu mwanzo wa mwaka wa fedha ili kutoa taarifa na ufafanuzi utakaosaidia kupunguza hoja za ukaguzi na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa, amewataka watendaji na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kuendelea kushirikiana, kuwa na uelewa wa pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa mshikamano ili kuepusha migogoro inayoweza kudhoofisha utoaji wa huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!